Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Halima Mdee akamatwa na Polisi

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amekamatwa na polisi wanne na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay saa  moja iliyopita.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo, amezungumza majira ya  saa 12 jioni na kueleza kuwa Mdee amekamatwa akiwa nyumbani kwake Makongo Juu.

 Awali akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi,  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi aliagiza Jeshi la Polisi kumkamata mbunge huyo  kwa madai kuwa amemkashifu Rais John Magufuli.

Kamanda wa Polisi, mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda amesema amefanya  hivyo kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya.

“Wapi kakamatwa? Sisi tunachojua ni kuwa tunatekeleza agizo la DC (mkuu wa wilaya) mengine muulize kamishna wa kanda maalum, nimetimiza,” amesema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top