Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano kutoka Chama cha Soka mkoani Mwanza MZFA Kess Mziray, Mratibu wa Mashindano ya Ndondo Cup Yahaya Mohamed, Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire pamoja na Mwakilishi wa jeshi la polisi mkoani Mwanza, SP.John Kafumu.
Na George Binagi @BMG
Baada ya mashindano ya soka ya Ndondo Cup kufanya vizuri Jijini Dar es salaam kwa miaka mine sasa tangu kuanzishwa kwake, mashindano hayo pia yamezinduliwa katika Jiji la Mwanza kwa ajili ya kutoa fursa kwa vijana kuonesha uwezo wao wa kusakata kabumbu.
Mratibu wa mashindao hayo yalioanza kutimua vumbi mwaka 2014 baada ya kuasisiwa kwenye kipindi cha Sports Extra cha Clouds Fm, Yahaya Mohamed amezungumzia ratiba kamili ya kuanza kwa mashindano hayo Jijini Mwanza.
Uzinduzi wa mashindano ya Ndondo Cup 2017 mkoani Mwanza, mbele ya wanahabari ambapo timu shiriki zimetakiwa kujisajili kwenye ofisi za Chama cha Soka mkoani Mwanza MZFA
Kutoka kushoto ni ripota wa Clouds Fm Mwanza Fabian Fanuel, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano kutoka Chama cha Soka mkoani Mwanza MZFA Kess Mziray, Mratibu wa Mashindano ya Ndondo Cup Yahaya Mohamed, Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire pamoja na Mwakilishi wa jeshi la polisi mkoani Mwanza, SP.John Kafumu.
Post a Comment