Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Matajiri wakubwa 10 Duniani



 Jeff Bezos.

Mwanzilishi wa Kampuni ya Amazon, Jeff Bezos amempita Bill Gates na kuwa tajiri namba moja duniani akimiliki utaji wa dola za kimarekani 90.6 bilioni (Tsh 203 trilioni).

Kupanda wa hisa za Amazon kwa asilimia 1.5 jana Alhamisi Julai 27, kulimaanisha kuwa tajiri huyo amempita mwanzilishi mwenza wa Microsoft, kwa mujibu wa taarifa za jarida la Forbes la nchini Marekani.

 Bill Gates.

Forbes wameeleza kuwa Bezos ana utajiri wa $90.6 bilioni akimzidi Bill Gates aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo akiwa na utajiri wa $90 billioni sawa na Tsh 201.5 trilioni.

Bezos ananakadiriwa kumilikia hisa milioni 80 za Amazon akiwa ni mwenye hisa nyingi zaidi ya mwingine yeyote.

Kwa miaka ya hivi karibuni amekuwa akijikita zaidi katika mradi wake wa Blue Origin unaohusika na urushaji wa rocket kwenda angani pamoja na Washington Post ambazo zote anazimiliki.

Warren Buffett.

Bezos ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu (CEO) wa Amazon alizaliwa mwaka 1964 Albuquerque Jimbo la New Mexico na alisoma Sayansi ya Kompyuta na Uhandisi wa Umeme katika Chuo Kikuu cha Princeton.
 Mack Zuckerberg

Alipohitimu alikwenda kufanya kazi na Wall Street lakini mwaka 1994 aliacha kazi na kwenda kuanzisha Amazon ambapo kwa mara ya kwanza Amazon ilianzishiwa katika karakana ya kutengenezea magari. Baada ya kampuni hiyo kuanza kufanikiwa na kujipanua katika nchi mbalimbali, mwaka 2000 alianzisha kampuni ya Blue Origin inayojishughulisha na masuala ya anga.

Michael Bloomberg.

Mwaka 2013 akiendelea kujipanua, aliinunua Kampuni ya Washington Post kwa $250 milioni na ilipofika Mei 2017 alitajwa kuwa na utajiri wa $ 84.8 bilioni, lakini leo Julai 27, 2017 amefikisha utajiri wa $90.6 bilioni na kushikilia usukani wa mtu tajiri zaidi duniani.

Kwa mujibu wa Forbes, hawa ndio matajiri 10 wanaoongoza duniani;

   Jeff Bezos (53)- Amazon.com

    Bill Gates (61)- Microsoft

    Amancio Ortega (81)- Zara

    Warren Buffett (86)- Berkshire Hathaway

    Mack Zuckerberg (33)- Facebook

    Carlos Helu (77)- telecom

    Larry Ellison (72)- software

    Michael Bloomberg (75)- Bloomberg LP

    Bernard Arnault (68)- LVMH

    Charles Koch (81)- diversified
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top