Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Anthony Mavunde amesisitiza nidhamu, uadilifu, bidii na kutokukata tamaa kwenye mafanikio ya ajira kwa vijana.
Mhe. Mavunde ameyasema hayo wakati akihojiwa na kipindi cha VijanaTz kinacholetwa kwenu na Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa kinachorushwa mubashara kupitia mitandao ya kijamii katika kurasa za UVCCM Instagram, Facebook na Twitter alisisitiza vijana wawe kwenye mkondo mmoja wa nidhamu na uadilifu.
“Vijana ndio nafasi yetu pekee ya kuonesha uwezo wetu kwa umma. Viongozi vijana lazima wawe na uwadilifu na nidhamu Natamani vijana wote tuwe kwenye mkondo wa nidhamu na uwadilifu” alisema Mhe. Mavunde.
Mhe. Mavunde alifafanua maana ya ajira kuwa ni shughuli yoyote ambayo inamfanya mtu ajipatie kipato halali kwa mujibu wa sera, sheria na taratibu zilivyo. Mhe. Mavunde ameeleza Serikali imesisitiza vijana kujikita zaidi kwenye ajira za kujiajili kuliko kutegemea ajira za kuajiliwa ambazo kimsingi Serikali imejikita kuwawezesha vijana kwenye Kilimo na Ufugaji ili kujipatia kipato pamoja ukuzaji wa vipaji.
“Serikali Tunaompango wa ukuzaji vipaji kwa vijana.Wizara imekuja na mpango wa miaka 5 kukuza vipaji kwa vijana wa Kitanzania. Pia imeleta mfumo mzuri zaidi wa kurasimisha ujuzi kwa vijana 3600” alisema Mhe. Mavunde.
Mhe. Mavunde alizidi kufafanua kuwa Serikali inategemea Viwanda kama silaha ya pili kufikia uchumi wa kati, ukiachia kilimo pia Serikali imeanzisha baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi, ambalo wanatoa mikopo na ruzuku.
Serikali imezidi kupambana na matatizo ya ajira ya vijana nchini kwa kufanya hatua za ziada za kuwafungulia kampuni vijana, kuajili vijana wa vyuo na kuwaongezea ujuzi kwa vijana wa kitanzania.
“Tunao vijana tuliowatoa SUA tukawatengenezea kampuni na sasa wanatoa ajira kwa vijana wenzao. Vijana wa vyuo watachukuliwa kupelekwa katika maeneo ya ajira serikalini. Pia Bunge limetutengea Tsh. Bilioni 15 kwaajili ya ukuzaji ujuzi kwa vijana wa Kitanzania” alisema Mavunde.
Mhe. Mavunde alibainisha Serikali kuona mapungufu ya vijana kwenye kuijua mifuko ya kijamii na asilimia kubwa wamekuwa wakikata tamaa pindi manafanikio yanapochelewa.
“Tunahaja ya kuendelea kutoa elimu kwa vijana wa Tanzania ili waelewe vizuri mifuko yetu. Vijana ndio moyo wa Taifa, tunapenda kuwaona vijana wengi wanatumia fursa na muda ipaswavyo. Kushindwa ni sehemu ya mafanikio, vijana wasikate tamaa” alisisitiza Mhe. Mavunde.
Usikose kuendelea kufuatilia kipindi cha #VijanaTz kupitia katika kurasa zetu za UVCCM Taifa.
*Imetolewa Na;
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi-UVCCM Makao Makuu*
#VijanaTz
Post a Comment