Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Shaka ashtukia mchezo mchafu UVCCMZipo taarifa zenye ushahidi wakina kwamba  wako watu wanaomaliza muda wao wa  uongozi katika jumuiya yetu wameanza kupanga safu nani achukue fomu wapi na nani achukue fomu wapi.

 Naendelea kuwakumbusha ndugu zangu kuwa anayetaka kupanga safu aende akapange nyanya sokoni na si uongozi ndani ya CCM na Jumuiya zake. CCM ina  hazina  ya kutosha ya vijana ambao wanaweza kuwa viongozi.

Anaepanga na  anaepangwa wakibainika wote watakula panga haiwezekani mtu mmoja  kujifanya ana hati miliki ya chama au jumuiya akaanza kupangia wenziwe safu ya  uongozi.

 Msiogope vijana jitokezeni kwa wingi kuomba nafasi hakuna aliyeandaliwa  kushika wadhifa fulani ndani ya jumuiya hii, chama chetu kina demokrasia pana sana tumieni haki na wajibu wenu wa kikanuni na kikatiba.

Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
01/07/2017

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top