Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Taarifa za upotoshaji kuhusu mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi

Kumekuwepo na upotoshaji wa mafunzo ya utarajali (Internaship programme) bila malipo yaani fedha za kujikimu wakati wa mafunzo hayo kwa baadhi ya wanaotarajia kuanza mafunzo kwa vitendo mapema mwaka huu.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kuwajulisha kwamba kwa sasa hakuna ‘intern’ aliyepangiwa kuanza mafunzo hayo kwani tunasubiri watoke waliopo kwenye mafunzo.

Barua iliyodukuliwa na kusambaa kwa lengo la kupotosha wataraji hao ilikuwa ni kwa ajili ya wataraji (intern) kutoka nje ya nchi ambao kwa sheria hawalipiwi na Serikali ya Tanzania.

Aidha wapo ‘intern’ wawili ambao wanasoma nchini China na mwingine Algeria masomo yao yalihitaji mafunzo kwa vitendo kabla ya kumaliza na kwa kuwa ilikua lazima warudi vyuoni mwezi Oktoba waliomba kufanya mafunzo hayo  kwa kujigharimia  pamoja na kuwa ni watanzania na wazazi wao walikuwa wameridhia hilo kwa maandishi ili warudi  mapema kumalizia program yao ya udaktari.

Hivyo ni watanzania wawili tu wameshapata barua yenye kuwataka  kujilipia kwa mazingira hayo hakuna wengine waliyepewa barua ya kuruhusiwa kwenda mafunzo ya utarajali (internship) bila malipo.

Imetolewa na;

Nsachris Mwamwaja
Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikali-Afya
30/7/2017
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top