Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TAKUKURU yanawasa Wagombea TFF ... Yupo Mtangazaji wa Clouds

Wagombea katika nafasi mbalimbali za uchaguzi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadau wa soka wamekatwa na TAKUKURU kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa jijini Mwanza.

Miongoni mwa waliyokamatwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), Almas Kasongo, Shafii Dauda  ambaye pia ni Mtangazaji wa Clouds Media Group, Elias Mwanjale, Leonald Malongo, Effam Majinge, Osuri Kasuli, Richard Kayenzi, Lazack Juma pamoja na Kelvin Shevi.

Hayo amebainisha Msemaji wa Takukuru Ernest Makale na kusema waliwakamata watu hao kwa kuweka mitego sehemu wanazofanyia vikao vyao vya siri.

"Tumewakamata kwa sababu hiki siyo kipindi cha kampeni na dalili zote kwamba walikuwa hapa kwa ajili ya uchaguzi unaotarajiwa zilikuwa zipo wazi, kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa tumeona kuna viashiria vya rushwa, tukaweka mitego katika sehemu walizokuwa wanaendesha vikao vyao vya siri tukaweza kuwakamata", amesema Makale.

Pamoja na hayo Makale amesema watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana ila wanaendelea na uchunguzi wao endapo watakapopata ushahidi wa kutosha watafikishwa mahakamani.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top