Kaimu Katibu Mkuu Umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiagana na na wanachama na viongozi wa chama na jumuiya zake mara baada ya mkutano wa ndani uliofanyika kata ya nyampulukano wilayani sengerema mkoa wa mwanza.(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)
Kaimu Katibu Mkuu Umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC)(Kushoto)akisalimiana na Katibu wa CCM wilaya ya Sengerema Ndg:Iddy Mkowa alipowasili katika katika ziara yake ya kikazi wilayan humo.
Kaimu Katibu Mkuu Umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC)(Kushoto)akisalimiana na kukaribishwa wilaya yaSengerema na Mwenyekiti wa UVCCM Bi:Magreth alipowasili katika katika ziara yake ya kikazi wilayan humo.
green guard wakimvika Skafu
Kaimu Katibu Mkuu Umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza mara baaada ya kukagua Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji cha vijana bwawani mazingira kata ya ibisabageni wiolayani sengerema mkoani mwanzaKaimu Katibu Mkuu Umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) (wa pili kushoto)akiwasili na kupokelewa ka shangwe na wanafunzi wa Shule ya sekondari wilayani sengereme
Na Mathias Canal, Sengerema
Watendaji wanaohudumu serikalini wametakiwa Kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015-2020 kwani wapende ama wasipende ni lazima watekeleze.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Wakati wa Ziara yake ya kuimarisha Chama Wilayani Sengerema.
Shaka Alisema kuwa kuna Watendaji ambao wameshindwa Kusimamia ipasavyo ilani ya Uchaguzi kwa sababu ya itikadi za kisiasa jambo ambalo linachelewesha Maendeleo endelevu kwa Wananchi na jamii kwa ujumla wake.
Alisema kuwa Watendaji wengi serikalini wameshindwa kuwajibika ipasavyo jambo ambalo limepelekea kwa kiasi kikubwa kukigombanisha Chama na Wananchi wake.
Katika Ziara hiyo ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kuimarisha Chama katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu wa Chama na Jumuiya zake Shaka ametembelea pia vikundi Mbalimbali vya Vijana ambavyo vimesajiliwa na kuanza shughuli za kujikwamua kiuchumi ikiwemo ujasiriamali.
Shaka Alisema kuwa ameamua kufanya Ziara hiyo katika Mikoa Mbalimbali nchini ili kuimarisha Chama na Jumuiya zake kwani umakini wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unajengwa na vikao Mbalimbali vya ndani ya Chama.
Aidha, Alisema kuwa kwa mujibu wa sheria Wananchi wanapaswa kusomewa taarifa za mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu ili kuondoa sintofahamu ya matumizi ya fedha za umma.
Shaka Alisema kumekuwa na matatizo makubwa katika maeneo Mbalimbali ya Upatikanaji wa Maji jambo ambalo Serikali inaendelea kulifanyia kazi kwa ajili ya kutatua jambo hilo.
Aliongeza kuwa kazi inayofanywa na vyama vya upinzani ya kuitupia serikali lawama na kupotosha wananchi bila kusema ukweli wa mazuri yafanywayo haitawaacha salama katika siasa za kipindi hiki kwani usimamizi mzuri wa Rasilimali za umma unaofanywa na Rais Magufuli ni njia pekee ya kupoteza kabisa Upinzani nchini..
Post a Comment