Mbunge Juliana Shonza
Habari kutoka mjini Dodoma zinaeleza kuwa wabunge kadhaa wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambao walikwazika na uchangiaji wa mbunge wa CCM Juliana Shonza na kutaka kumpiga wakati mbunge wa Kawe Halima Mdee alipokuwa akipewa adhabu kwa kutoa lugha chafu bungeni wamekamatwa .
Taarifa zilizoufikia zinadai kuwa wabunge hao walikamatwa jana majira ya usiku baaada ya bunge kuarishwa na baada ya kukamatwa walifikishwa polisi na bado haijajulikana iwapo waliachiwa ama lah.
Idadi ya wabunge waliokamatwa inasadikika kufikia zaidi ya watano ,mtandao huu unaendelea kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma ili kuthibitisha kukamatwa kwa wabunge hao. |
Post a Comment