Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waziri Mbarawa awanyooshea kidole TAA


Profesa Makame Mbarawa ,Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuweka mikakati endelevu ili kuwezesha kiwanja cha ndege cha Tabora kujisimamia na kujiendesha kutokana na miundombinu bora na ya kisasa inayoendelea kujengwa kiwanjani hapo.

Amezungumza hayo jana mkoani humo, mara baada ya kuanza ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine Waziri Profesa Mbarawa amekagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanja hicho ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 96 na umegharimu kiasi cha Sh 27bilioni.

"Hivi sasa huduma ya usafiri wa ndege katika kiwanja hichi unaridhisha, hivyo ongezeni ubunifu ili kuvutia abiria wengi na kuwezesha kiwanja kujiendesha", amesema Profesa Mbarawa.

Amesisitiza kuwa gharama za usafiri wa anga zitaendelea kupungua kadri huduma na ubora zitavyokuwa zinaendelea kuongezeka ili kuwezesha abiria wengi zaidi kutumia usafiri huo na hivyo kuwezesha pato la Taifa kuongezeka.

Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege mkoani Tabora  Mhandisi Danstan Komba amemueleza waziri kuwa idadi ya abiria wanaotumia kiwanja cha ndege hicho imeongezeka kutoka asilimia 10 kwa mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 62.3 mwaka 2016 kutokana na ndege za ATCL kuanza safari zake mkoani humo.

Ameongeza kuwa baada ya mradi wa ujenzi wa kiwanja hicho kukamilika, mashirika ya ndege yataongeza safari zake mkoani humo kwa kuzingatia uwepo wa miundombinu bora yenye kukidhi mahitaji na hivyo itatoa chachu ya maendeleo kwa wakazi wake  na kuboresha shughuli za kiuchumi na kijamii.

Naye, Meneja wa Mradi wa ujenzi wa kiwanja hicho Mhandisi Neema Joseph, amemuahidi Waziri  Mbarawa kumsimamia mkandarasi kumalizia kazi zilizobaki uwanjani hapo ndani ya siku 14 na kwa kuzingatia viwango na ubora.

Katika hatua nyingine, Waziri  Mbarawa amezungumza na viongozi na wafanyakazi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake na kusisitiza kufanya kazi kwa kuzingatia uaminifu, weledi, kasi na uzalendo ili kuendeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta maendeleo kwa wananchi wake na kufikia uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

Waziri Mbarawa yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili ya kukagua miradi ya miundombinu iliyopo mkoani Tabora.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top