Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wema atoa povu zito kwa wanaopiga picha za ujauzito

Ni kawaida kwa baadhi ya wanawake hasa mastaa kupiga picha wakati wa ujauzito kwa ajili ya kumbukumbu zao na wakati mwingine kutokana na mapenzi waliyonayo kupiga picha ambapo mastaa mbalimbali wa kike duniani wamekuwa wakifanya hivyo.

Jambo hilo pia tumekuwa tukilishuhudia hata hapa Tanzania na baadhi ya mastaa pia wameshawahii kupiga picha za namna hiyo na wakati mwingine kuziweka kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo baadhi ya watu linawakera.

Wema Sepetu ni mmoja wa watu ambao wameonesha kukerwa na kitendo hicho akisema ni ukiukwajii wa maadili ya kiafrika na watanzania kwa ujumla na kuutumia ukurasa wake wa Instagram  kumpongeza muigizaji wa Bongomovie Esha Buheti baada ya kupiga picha akiwa mjamzito ndani ya mavazi ya kumsitiri.

Wema ameongeza kwa kusema kuwa ameshakubaliana na hali yake ya kutoweza kupata mtoto lakini hiyo haimzuii kusema yanayomkera kuhusiana na mambo ya uzazi.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top