Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAKONDA AWAONGEZEA NGUVU TBC







Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam *Paul Makonda* leo ametoa msaada wa *Gari* aina ya *Noah*, *Pikipiki* Tatu, *Computer* Tano na *Camera* Mbili za kisasa kwa Shirika la Utangazaji Tanzania *TBC* ili kuongeza nguvu katika kuwafikia Wananchi.

Mbali na Vifaa hivyo vya kisasa pia *Makonda* amefanikiwa kumpata mfadhili atakaepaka Rangi Jengo lote la *TBC* kuanzia siku ya kesho ili liwe na mwonekano wa kisasa.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo *MAKONDA* amesema lengo ni kuwawezesha Wananchi ambao hawana uwezo wa kuita vyombo vya habari na kueleza matatizo yao waweze kufikiwa.

Makonda ametoa msaada huo baada ya kufika Ofisi za TBC na kubaini uwepo wa changamoto za vifaa ikiwemo Usafiri, Camera na Computer ambapo kwa sasa *Gari* na *Pikipiki* hizo zitawawezesha Waandishi kufika kwenye matukio kwa uharaka huku*Compute* zikimuwezesha  M
Wahariri kutekeleza majukumu yao.

*Vifaa* hivyo vitatumika kuongeza nguvu kwenye kipindi cha Hadubini ambacho kimekuwa kikisaidia Wananchi wanyonge kupaza sauti zao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa *TBC * Bi. MARTHA SWAI* amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwapatia msaada huo kuku *Zaitun Mkwama* ambae ni mtayarishaji wa kipindi cha Hadubini akieleza kuwa vifaa hivyo vitawaongezea ufanisi katika kazi yao.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top