Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Prof. Mkumbo ampongeza Raila Odinga

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo amepongeza hatua zilizochukuliwa na kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga za kwenda mahakamani kudai haki yake.

Amesema kuwa kipindi ambacho kina Odinga wanapambana kupigania mageuzi wakati wa muhula wa pili wa utawala wa Rais Daniel Arap Moi, Uhuru Kenyatta yeye alikuwa kivulini

Prof. Mkumba amesema kuwa Raila Odinga ni mwanasiasa aliyekomaa kidemokrasia hivyo anafaa kuitwa baba wa demokrasia barani Afrika huku akiwataka wanasiasa kuiga mfano huo.

“Ahsante sana Raila Odinga kwa hakika maamuzi uliyofanya kwenda mahakamani kutafuta haki ni maamuzi sahihi, wewe ni baba wa Demokrasia katika ukanda huu,”amesema Prof. Mkumba.

"Huyu Kenyatta ni beneficiary. Wakati akina RAO wakipambana na akina Moi yeye alikuwa kivulini. Tuwe wa kweli"amesisitiza Kitila Mkumbo 

Uchaguzi mkuu nchini Kenya umefanyika hivi karibuni ambapo mgombea kutoka chama tawala cha Jubilee, Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi na kumbwaga Raila Odinga 

==>Chek apo chini
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top