Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SERIKALI KUANZA KUTOA LESENI MPYA KWA MAGAZETI NA MAJARIDA NCHINI


SERIKALI imesema inaanza kutoa leseni mpya za machapisho mbalimbali ikiwemo magazeti na majarida yote nchini ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kifungu cha 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 unaokwenda pamoja na Kanuni ya 7 ya Kanuni za Sheria ya Huduma za Habari za mwaka 2017 zilizochapishwa kwa mujibu wa tangazo la Serikali na 18 la Februari 3, 2017.

Akizungumza katika Mkutano na Wanaandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema kuwa utoaji huo wa leseni kwa machapisho yote umeanza rasmi leo Agosti 23, 2017 na utafikia tamati Octoba 15, 2017 na magazeti yote yahakikishe yanakamilisha taratibu ya kupatia leseni mpya kwa kipindi hicho, na baada ya muda huo hawataruhusiwa kuyachapisha kwani watakuwa wanatenda kosa kisheria.


Dkt. Abbas amesema, kwa mujibu wa sheria, utaratibu huu wa sasa unafuta mfumo wa awali wa utoaji wa Hati za Usajili wa magazeti na majarida uliokuwa ukitumika kwa mujibu awali kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.

Fomu za maombi, akaunti ya kulipia pamoja na orodha ya nyaraka zinazohitajika kwa ajili ya usajili huo, vinapatikana kuanzia saa katika ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO za jijini Dar es salaam na Dodoma au katika sehemu ya "Huduma Zetu" katika tovuti ya Idara hiyo BOFYA HAPA.
Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas akizungumza katika Mkutano na Wanaandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top