Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Shaka afanya mazungumzo na RC Iringa

Sehemu ya kauli zilizotamkwa na Kaimu Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza ofisini kwake mjini Iringa alipokutana nae kufanya mazungumzo ya kuimarisha mahusiano baina ya UVCCM na Serikali ya Mkoa leo 10/08/2017
*Dhamira  njema ya UVCCM kukifufua chuo hiki ni kuendelea kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Serikali ya awamu ya Tano na kifikra na Falsafaza katika uchumi wa viwanda , Uadilifu, ushapakazi, uzalendo na ujasiriamali za Mwenyekiti wa CCM Mhe. Dr. John Pombe Magufuli.
*Hakuna taifa lolote lile Duniani lenye uwezo wa kuwapatia vijana wote Ajira,Tumedhamiria kukifufua chuo hiki  ili vijana wenzetu tuwapike na kuwafundisha stadi za maisha, ujasiriamali, ufundi,  uzalendo,  siasa na Itikadi ya chama chetu.
*Hii itawawezesha vijana kuendesha miradi yao kwa ufanisi zaidi.
*UVCCM imedhamiria kwa dhati kuwapika na kuwaoka vijana katika fani za uongozi na maadili na uzalendo kwa Taifa na kwa chama cha Mapinduzi.
*Fursa hii itawawezesha vijana kuandaliwa kisaikolojia, kujitegemea na kuendesha biashara zao kwa ufanisi na kwa uadilifu wa hali ya juu.
*UVCCM imeona njia pekee ya kumuunga mkono Mhe Rais. Dk. John Pombe Magufuli ni kuinua maisha ya vijana dhidi ya umasikini na matumizi bora ya rasilimali za taifa.
*Nguvu kazi ya Taifa ni vijana wenyewe kujitambua, kujituma na
kujitegemea kisera, mipango chini ya programu  nzuri za serikali ya awamu ya tano za kutaka kurudisha uzalendo, ufanisi kiuchumi, kisiasa na Kijamii pamoja na Fikra sahihi na chanya za kizalendo za Muasisi wa Taifa Letu Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius K. Nyerere zimetusukuma UVCCM kufikiri upya umuhimu na ulazima wa kukifufua  chuo hiki cha mafunzo kwa namna bora na endelevu ili kukifanya kiwe kituo Rasmi kitakachotumika kuwapika na kuwaandaa vijana wa CCM kupitia mafunzo ya itikadi, maadili, Uzalendo na Uchapakazi utakaosaidia kuinua na kustawisha Tanzania Mpya na CCM Mpya kwa kipindi cha sasa na baadaye.
Mapema Kaimu Katibu Mkuu  Shaka Hamdu Shaka alitembelea na kukagua hatua za mwisho za maandalizi ya  marekebisho ya chuo cha UVCCM Ihemi Iringa ambacho kinatarajiwa kuanza tena kutoa mafunzo kwa vijana mapema mwezi Septemba mwaka huu.
MWISHO
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top