Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Uamuzi wa CUF kwa Maalim Seif

Chama cha CUF kimedai kuwa, licha ya uwepo wa hujuma zinazofanywa na baadhi ya watu ili kumuondoa madarakani Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, katibu huyo ataendelea kubaki kwenye nyadhifa yake hadi pale Mkutano Mkuu halali wa CUF utakapotengua ukatibu mkuu wake.

Akizungumza na waandishi wa habari,  Agosti 5, 2017 jijini Dar es Salaam, Kaimu Naibu Katibu Mkuu CUF, Joran Bashange alidai kuwa baadhi ya taasisi za serikali zinafanya hujuma ya kutotambua maamuzi ya Maalim Seif kwa lengo kumfanya Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na maamuzi yake kutambulika kwenye taasisi hizo.

“Mpaka tone la damu la mwisho linatokea, Katibu Mkuu ataendelea kubaki katibu hadi pale mkutano mkuu wa chama utakapobadilisha maamuzi hayo. Taasisi hizo hazimtambui kwa maneno lakini kisheria zinamtambua hata mahakama zinamtambua Maalim Seif kuwa Katibu Mkuu wa CUF,” alisema na kuongeza.

“Maamuzi yote anayofanya Lipumba yanaratibiwa, ili kuiondoa CUF. Seif ametuma barua nyingi za kusimamisha uanachama baadhi ya watu lakini Ofisi ya Msajili haitaki kuzifanyia maamuzi.”

Bashange alidai kuwa, Maalim Seif ataendelea kutekeleza majukumu yake.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top