Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waziri Mwijage Aivaa TRA ..... Aitaka Isimfanye Akatumbuliwa na Rais

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutomfukuzisha kazi kwa uzembe wao uliopelekea nchi kupigwa na kupata hasara kutokana na watu kuingiza cement kutoka nje ya nchi wakidai ni krinka.

Waziri Mwijaga alisema hayo jana kupitia kipindi cha HOTMIX na ambapo alitumia nafasi hiyo kupiga marufuku Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kukagua krinka yoyote kutoka nje ya nchi.

"Mtu anatengeneza Krinka anauza Kenya, sasa kama mtu anatengeneza Krinka Tanga anauza Kenya wewe unafuata nini Pakistan? Hakuna krinka inatoka nje ya nchi ile ni Cement iliyokamilika TRA wanashindwa kufanya kazi yao, narudia kusema hakuna krinka inaingia nchini kutoka nje ile ni Cement kamili na anayepinga aje aniambie mimi, na kuanzia leo TBS wasikague krinka yoyote kutoka nje ya nchi waingize ndani ya nchi bila TBS kukagua, TBS ipo chini yangu sasa kama mimi naambiwa sitoshi na wa TBS ajiangalie" alisema Mwijage

Aidha Waziri Mwijage alidai kuwa watu wa Cement walikubaliana na DR Meru kununua hizo Krinka hapa hapa nchini

"Watu wa Cement walikubaliana hapa na Dr. Meru, Twiga Cement ananunua Krinka, Simba Cement ....mwingine nani ananunua krinka nyingine kutoka wapi, watu wanaleta cement iliyokamilika wanasema Krinka sasa kuanzia leo TBS hawezi kukagua krinka yoyote kutoka nje ya nchi, mpaka mamlaka iliyopo juu yangu sasa kama TRA walizembea tukapigwa juu yao kwanini wanataka kuniharibiana kazi, eti bwana wanataka kuniharibia kazi mimi" alisisitiza Waziri Mwijage
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top