Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

AFISA MSAIDIZI WA FORODHA ALIYEISHI KIFAHARI, KAFIKISHWA MAHAKAMANI.


Afisa msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kumiliki mali ambayo ni magari 19 na kuishi maisha ya kifahari kinyume na mshahara wake.

Mshtakiwa alisomewa makosa yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi na Wakili wa Serikali, Vitalis Peter ambaye alidai mshtakiwa ana makosa mawili.

Alidai kuwa kati ya March 21, 2016 na June 30, 2016 katika maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam, akiwa mwajiriwa wa TRA, kama Afisa Msaidizi wa Forodha alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake, kinyume na sheria.

Inadaiwa alikutwa akimiliki magari 19 ambayo ni Toyota RAV4, Toyota Dyna Truck, Toyota Vitz, Suzuki Carry,Toyota Ipsum, Toyota Wish,Toyota Mark ll, Toyota Regiusage, Toyota Estima, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota Crown, Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Lasso, Suzuki Carry, ambayo yana thamani ya Tsh. Milioni 197.6.

Kosa la pili, anadaiwa kuwa kati ya March 21, 2012 na March 30, 2016 jijini Dar es Salaam akiwa mwajiri wa TRA aliishi maisha ya kipato cha juu tofauti na kipato chake yenye thamani ya Tsh. 333,255,556.24 tofauti na kipato chake.

Wakili Peter amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, hivyo anaomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali (PH).

Hata hivyo, upande wa utetezi kupitia Wakili Elisalia Mosha aliiomba Mahakama hiyo kumpa dhamana mteja wake kwa sababu mashtaka aliyonayo yanadhanika kisheria.

Hakimu Shaidi alimtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Tsh. Milioni 20 ambapo alikidhi masharti na kuachiwa kwa dhamana.

Kesi imeahirishwa hadi November 7, 2017.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top