Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Vijana watuma Salamu nzito kwa Rais Magufuli






*21/ 10/2017 Mkoa wa Dodoma*

*KAULI MBIU:  UTAIFA NA UZALENDO KWANZA  LINDA RASILIMALI ZA NCHI.*
----------------------------------------
Leo Jumamosi 21 Oktoba 2017 Vijana wazalendo wamewakilisha vijana wenzao toka mikoa na wilaya zote za Tanzania kuwasilisha tamko rasmi  lililobeba ujumbe maalum kuenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Joseph Pombe  Magufuli.

Tamko hilo lilikabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe  Jordan Rugimbana na Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka kwa niaba ya vijana wote wa Tanzania ambao walisaini tamko hilo.

Vijana waliosaini ni kutoka vyama vya siasa chadema, Act wazalendo, TLP, CUF, DP,     NCCR Mageuzi, vijana wa bodaboda, mama lishe, machinga, vijana toka vyuo vyote vilivyopo Dodoma na vijana wengine wakiwakilisha wilaya na mikoa yote ya Tanzania

Aidha  viongozi wa  dini katika tukio hilo waliongoza *sala na maombi* kumuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Joseph Pombe Magufuli

Tuko hilo kubwa na la historia limehudhuriwa pia na Naibu Waziri (OWM) Vijana kazi na watu wenye ulemavu Antony Mavunde, madiwani, wabunge, na viongozi wa dini, Vijana kutoka maeneo mbali mbali lilifanyika katika ukumbi wa mikutano Dodoma Hotel.

Kauli mbiu ya shuhuli hiyo ya mabadhiano ya tamko maalum  la vijana ni:

*Utaifa na uzalendo kwanza Linda Rasilimali za Nchi.*

*TAARIFA RASMI YA VIJANA ILIYOBEBA UJUMBE MAALUM KUENDA KWA MHE. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KUTOKA KWA VIJANA WA MAKUNDI YOTE NCHINI, JUMAMOSI 21 OKTOBA 2017,  MBELE YA MKUU WA MKOA WA DODOMA, ILIYOWASILISHWA NA NDG. SHAKA HAMDU SHAKA KWA NIABA YA VIJANA WA TANZANIA.*

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Mhe, Naibu Waziri wa (OWM) Kazi, Vijana na watu wenye Ulemavu,
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini
Waheshiwaa Wabunge, Madiwani, Viongozi wa Vijiji, Vitongoji. Viongozi mbali mbali wa Vyama Vya Siasa
Viongozi wa Madhebu mbali mbali ya dini mliohudhuria
Ndg Vijana wenzangu toka maeneo mbali mbali ya Tanzania.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa.
 Kwa heshima kubwa tumelazimika kukutana hapa kwa lengo moja kuu na maalumu lenye kujali maslahi mapana ya nchi yetu. Mkusanyiko wetu huu wa leo sisi Vijana wazalendo wa Tanzania toka Mikoa mbali mbali, bila kujali itikadi za vyama vyetu na makundi tofauti ya kijamii  baada ya majadiliano na makubaliano ya pamoja, tumeona ipo haja ya kutanguliza mbele utaifa na uzalendo kwa nchi yetu.

Tumekutana hapa Dodoma ili kuithibitishia dunia kuwa tumeridhishwa na utendaji unaopigania maslahi ya wananchi masikini na wanyonge unaofanywa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na  Rais Dk John Joseph Pombe Magufuli.

Baada ya kukupatia ujumbe wetu maalum wa kimandishi, tutakuomba ndugu Mkuu wa Mkoa umfikishie Mheshimiwa Rais mezani kwake ili ajue na atambue jinsi Vijana wa Tanzania kutoka makundi mbali mbali  tunavyomuunga mkono katika juhudi zake za kupigania maendeleo endelevu nchini kwa kusukumwa na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa.
Sisi vijana tumekusanyika hapa tukiwa tumebeba  kauli mbiu ya Utaifa na Uzalendo kwanza Linda Rasilimali za Taifa, ndio maana leo tukakuomba wewe Mheshimiwa  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma uwe shuhuda wa kuona jinsi tulivyoguswa na  ujasiri wa Mheshimiwa Rais wetu.

Mungu ameijaalia na kuibariki nchi yetu  kuwa na rasilimali nyingi kama madini, maliasili, mbuga, wanyamapori, mito, maziwa, bahari na fukwe nzuri ambazo ni utajiri kwa maendeleo ya binadamu wote na si tabaka fulani ndilo lifaidike.   Lengo letu hafla hii fupi ya uzalendo ni kupongeza ujasiri na uthubutu ulioonyeshwa na Rais wetu kwa jinsi anavyobeba dhima na jukumu la kupigania maslahi ya Taifa ili kupata maendeleo ya pamoja.   Zipo sababu nyingi muhimu zenye maana, mantiki, mashiko na za msingi ambazo zinaelezeka mbele ya kadamnasi  nchini mwetu, Afrika Mashariki, Bara zima la Afrika na dunia kwa ujumla .

Sisi vijana tumeridhishwa kwa asilimia 100 kuwa Rais Dk John Pombe Joseph  Magufuli amekuwa ni kioo kinachoakisi uhalisia unaojali shida za wananchi wake huku akihimiza kila wakati na kututaka sisi wananchi tuweke mbele uzalendo na kujivunia utaifa wetu.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa.
Mkusanyiko wetu huu umejumuisha makundi mbali mbali  baada ya kujadiliana kufanya tathmini yakinifu hatimaye tumetoka na msimamo wa pamoja kifikra kwa kuheshimu misingi ya uzalendo na utaifa wetu.
Kila mtanzania leo ni shahidi mzuri kwa yale yote yanayofanywa na kutekelezwa kwa vitendo na serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dk John Pombe Joseph Magufuli. Rais wetu amekuwa mzalendo na mtetezi aliyejitoa muhanga kuwatumikia watu wanyonge na masikini lakini pia akiwa na kusudio la kupigania maslahi ya Taifa.
Hakuna shaka yoyote aina ya uongozi wake umebeba dhima na hisia ya uzalendo wenye afya halisi kwa maendeleo ya pamoja .

Mheshimiwa  Mkuu wa Mkoa
Tunaendelea kusisitiza kuwa mkusanyiko wetu huu vijana  hauna maana nyingine yoyote ile au wenye kutoa tafsiri isiofikirika ingawaje wapiga dili na wezi wa mali za umma hawataridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano.
Sisi vijana wa nchi hii kwa niaba ya wenzetu wengine, hatuko na hatutakuwa tayari kupuuza juhudi, kujitolea kwa kiongozi wetu mkuu na michango yake inayokuza ufahamu wa maarifa ya kuthamini dhana ya utaifa wetu na uzalendo. Rais Dk John Pombe Magufuli ameidhihirishia dunia kuwa amekataa kuwa mtumwa wa fikra, hataki kukumbatia ukoloni mamboleo na anayewanyenyekea mabeberu na wayonyaji.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa.
Hatukuja hapa ili kufanya mahubiri ya siasa. Tumekusanyika kwa nia moja ya kuhimiza haki hatimaye salamu zetu zifike kila pembe ya nchi yetu na dunia huku tukipaisha sauti zetu kwa niaba ya Vijana wenzetu wote wa Tanzania tutaendelea kuwa bega kwa bega, kuhimizana kufanya kazi za uzalishaji kwa bidii ili kupambana na umasikini wa kipato, tutaendelea kupiga vita adui ujinga na maradhi ili kuwa na taifa imara na tutaendelea kumlinda na kumtetea Mheshimiwa Rais wetu dhidi ya wote wasiomtakia mema na kulitakia mema Taifa letu.

Tumeamua kumuunga mkono kwa dhati Rais wetu kutokana na ushupavu alionao, ujasiri wake, uchungu na mapenzi kwa nchi yake hasa katika kupigania maslahi ya umma akitaka yawanufaishe wananchi masikini na wanyonge
Kwa kauli moja kwemye tamko  hili la uzalendo tumeazimia:

Tunaipongeza Serikali ya Rais Dk John Pombe Magufuli kwa umakini, uwajibikaji na utetezi wa maslahi ya wananchi masikini na wanyonge.
Tumeridhishwa na juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika kudhibiti vitendo vya wizi, ukwapuaji mali na ubadhirifu wa mali za umma.
Washiriki katika tamko hili la uzalendo wamejiridhisha kufuatia mkakati wa serikali kushughulikia masuala ya uchimbaji madini na kulinda rasilimali utasaidia kuongeza nafasi za ajira kwa wazawa (Vijana) tofauti na hapo awali.
Vijana tunaipa mkono wa heko Serikali kwa kuanzisha mazumgumzo na Wawekezaji wa Barrick Gold Mine na kufikia maamuzi ya haki na usawa katika mgao wa  faida utokanao na mapato ya madini .
Vijana wote wazalendo wa Taifa hili tutaendelea kumpongeza na kumtia shime Mhe Rais John Pombe Magufuli kwa kutokubali kurudi nyuma katika vita mbali mbali vya uchumi anavyovianzisha vyenye lengo la kulinda maslahi na heshima ya watanzania tokea aingie madarakani katika kupigania maslahi ya umma.
Sisi Vijana tumejiridhisha na Tunamuomba  Mhe, Rais na serikali yake waendelee na mkakati wa kuirudishia heshima nchi yetu kwa kulinda rasilimali zake.
Sisi Vijana tunamuona Mhe Rais Dk Magufuli akifuata nyayo za waasisi wa ukombozi wa Afrika waliojitolea muhanga kupigania uhuru na kutaka mali za Afrika ziinufaishe Afrika na watu wake, hivyo tutaendelekwa  pamoja kumuombea kwa Mwenyezimungu amlinde na kila mabaya.
Vijana wa Tanzania tutaendelea kumuunga mkono Rais Dk Magufuli usiku na mchana kwa hatua anazozichukua za kupambana na maadui ujinga, umasikini maradhi huku akitaka Taifa lijitegemee kiuchumi na kimaendeleo.
Mwisho kwa niaba ya vijana wenzetu tunaijuilisha na kuitangazia dunia kuwa Tanzania siyo shamba la bibi toka sasa Serikali itasimamia mali zake na kushirikiana na wadau wema wanaojali maslahi ya pamoja bila kutuimia mirija ya unyonyaji.

Baada ya maelezo hayo mafupi sasa naomba nikukabidhi warka uliosainiwa na vijana zaidi ya 500 wakiwakilisha wenzao kutoka mikoa na wilaya zote za Tanzania ukionyesha kuunga mkono na kuguswa na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dk John Joseph Pombe Magufuli.

Hakika Magufuli ni Zawadi kwa Watanzania toka kwa Mwenyezi Mungu.


Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top