Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Serikali yatoa pole kwa Clouds Media Group

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amepokea kwa mshtuko na masikitiko taarifa za ajali ya moto kwenye ofisi za  kituo cha Redio na Televisheni cha Clouds Media cha Jijini Dar es Salaam hapo jana.

Waziri huyo ambaye yuko mkoani Iringa kwa ziara fupi ya kikazi, ametoa pole kwa viongozi na wafanyakazi wa kituo hicho cha redio na televisheni kwa kuunguliwa na baadhi ya vifaa vya kazi vya chombo hicho cha habari na kuzitaka Taasisi husika kufanya uchunguzi wa kina kujua chanzo cha moto huo.

Aidha, Dkt. Mwakyembe amelipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini kwa kuitikia wito na kufika kwa haraka sehemu husika na hivyo kudhibiti moto huo usilete madhara makubwa zaidi.

Imetolewa na:
Lorietha Laurence
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
22/11/2017.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top