Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wakazi 1,172 wanufaika na mafunzo ya upanuzi wa makazi ya Rais



Dodoma. Jumla ya wakazi 1,172 wanaoishi katika vijiji vitano vilivyopo

jirani na Ikulu Chamwino mkoani hapa wamenufaika na mafunzo ya

kuwaongezea ujuzi ili  washiriki vyema katika upanuzi wa makazi ya

Rais.

Neema hiyo imefuatia utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli

alilolitoa Julai mwaka jana mjini hapa la Serikali kuhamia mkoani hapa

kabla ya awamu ya kwanza ya uongozi wake kukamilika.

Tayari Waziri Mkuu, mawaziri, manaibu, makatibu wakuu, manaibu

makatibu wakuu na baadhi ya watumishi wameshahamia mjini hapa ikiwa ni

utekelezaji wa agizo hilo.

Akizungumza katika mahafali ya tisa ya Chuo cha Veta mkoani hapa, Mkuu

wa chuo hicho Ramadhan Mataka amesema  kuwa mafunzo hayo yaliendeshwa

chini ya mfumo wa Competent Based Education and Training (CBET).

“Tumeshirikiana na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao

tumeshirikiana nao katika kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa baadhi ya

washiriki 1,172 kutoka katika vijiji vitano kwa lengo la kuwaongezea

ujuzi ili washiriki vyema katika upanuzi wa Ikulu ya Chamwino,” amesema

Mataka.

Mataka amesema  pia chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Kazi Ajira,

Vijana na Watu wenye Ulemavu wamewatambua wanagenzi 260 ambao kati ya

hao 241 wamefaulu baada ya kupimwa mkoani Dodoma.



Akizungumzia kuhusu programu hiyo ya wanagenzi, Naibu Waziri katika

Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana Antony Mavunde amesema  chini

ya programu hiyo wanawachukua wakufunzi wa Veta na kwenda nao mtaani

kwa ajili ya kubaini mapungufu waliyonayo vijana na kuyaziba.

“Baadaye vijana hao tunawapa vyeti vya Veta bila kusoma Veta. Hawa ni

vijana 3,900 ambao wako mitaani,”amesema
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top