Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WALEMAVU WALIOKIMBILIA KWA RC MAKONDA SASA WAANZA KUPATA NEEMA



Hospitali ya *CCBRT* imeguswa na Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam *Mheshimiwa PAUL MAKONDA* ya kutafuta Miguu Bandia kwa *watu wenye uhitaji* kwa kuwapatia matibabu *Wagonjwa 35* waliokatwa Miguu kutokana na *Ugonjwa wa kisukari.*

Miguu hiyo ya kisasa ina thamani ya zaidi ya *Shilling Million 157* ambapo Kati ya *Wagonjwa 35* waliokuwa wakitembelea *Magongo* kwa muda mrefu baada ya kukatwa miguu, *21 wameshawekewa Miguu Bandia na sasa wanaendelea na Shuguli zao* baada ya kuwa wazima.

*RC MAKONDA* amesema lengo la kampeni hiyo ni *kusaidia wanaotumia Magongo kupata Miguu ya Bandia ya kisasa ili waweze kuendelea na shughuli zao ujenzi wa Taifa* na kuhudumia Familia.

Ameishukuru *Hospital ya CCBRT* kwa kuunga mkono kampeni hiyo pamoja *E FM RADIO* na *TV E* walioojitolea kuhamasisha jamii kuchangia Miguu Bandia.

Katika hatua nyingine *RC MAKONDA* amepatiwa kiasi cha *Shillingi Million 10,000,000* kutoka kampuni ya Ujenzi ya *SPECTUM DESIGN* ambapo Mkurugenzi wake *Arch.JIMMY MKENDA* amesema lengo la kutoa mchango huo ni baada ya *kuguswa    na kampeni hiyo* inayolenga kuwasaidia *waliokata tamaa baada ya kupoteza miguu*.

Aidha *RC MAKONDA* amesema kuwa atazungumza na *Taasisi zinazotoa Bima ya Afya* ili waongeze kipengele cha *Matibabu na kutoa Miguu bandia* kwa watu waliopoteza Miguu kwa *Ajali au Ugonjwa.*

Amehamasisha jamii kuchangia kampeni hiyo kupitia *CRDB* account namba *0150299713500* au kufika ofisi za Mkuu wa Mkoa au E FM Radio kisha kuwasilisha mchango wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa walemavu Hospital ya CCBRT *BRENDA MSANGI* amewaasa *Wananchi kuchangia kampeni hiyo* huku akieleza kuwa *wataendelea kushirikiana na Mkuu wa Mkoa.*
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top