Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Magufuli awatoa gerezani Babu Seya na Papii Kocha

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, ametangaza msamaha kwa Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Jonson Nguza (Papii Kocha) ambao waliofungwa maisha katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam na kutaka waachiwe huru mara moja kutoka gerezani.

“Tanzania tuna jumla ya wafungwa 39,000 ambapo wanaume ni 37,000 na wanawake 2,000.  Wafungwa waliohukumiwa wako 522 kati yao wanaume ni 503 na wanawake ni 19. Nimeamua kusamehe wafungwa 8157, ambapo baada ya msamaha huu wafungwa 1828 watatoka leo.

“Mfano wa watu niliowasamehe ni Mzee Mganga Matonya mwenye umri wa miaka 85 amekaa Gerezani miaka 37 na miaka 7 ya kukaa mahabusu. Nimeamua kusaheme familia ya Nguza Viking jina lingine anaitwa Babu Seya na Ndugu Johnson Nguza ama Papii Kocha.

“Nimeamua kuwasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa. Lakini katika kuchunguzwa kwingi wapo wafungwa ambao wametubu dhambi zao, wamekiri makosa yao kwelikweli,” alisema Magufuli.

Mwaka 2003, Babu Seya na wanaye watatu walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kubaka na kulawiti watoto wa Shule ya Msingi Mashujaa, mwaka 2004, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar iliwahukumu wote wanne kifungo cha maisha jela.

Baada ya hukumu hiyo, walikata rufaa lakini mwaka 2005, Mahakama Kuu iliridhia hukumu hiyo ya kifungo cha maisha jela kwa wote wanne kabla ya Mahakama ya Rufaa kuwaachia huru Mbangu na Chichi Februari 2010.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top