Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAVUNDE AAGIZA WAAJIRI MWANZA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSHINDWA KUJISAJILI MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI-WCF


 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akiwa kwenye ziara yake  mkoani Mwanza kukagua Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa Agizo la Mhe.Waziri Jenister Mhagama.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza katika ukaguzi wa viwango vya kazi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza katika ukaguzi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akikagua nyaraka mbalimbali.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akiwa kwenye ziara yake  mkoani Mwanza kukagua Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa Agizo la Mhe.Waziri Jenister Mhagama.
............................................................
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde ameagiza Wakurugenzi wa Kampuni ya  Ujenzi ya JASCO LTD,AIRCO na JB BELLMONT HOTEL kufikishwa Mahakamani kwa kushindwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF).

Mavunde ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake katika mkoa wa Mwanza kukagua Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa Agizo la Mhe.Waziri Jennister Mhagama ambaye aliwataka waajiri wote nchini wawe wamejisajili kwenye mfuko wa Fidia wa Wafanyakazi kabla au ifikapo 30.09.2017.

Katika Mkoa wa Mwanza, Mavunde amesema jumla ya waajiri takribani 700 hawajajisajili katika mfuko wa Fidia wa Wafanyakazi ambapo zoezi la msako wa waajiri hao litaendelea kwa wiki nzima na kuwachukulia hatua stahiki wale waajiri wote wataokuwa hawatii matakwa ya sheria ya Fidia ya Wafanyakazi.

Kwa mujibu wa Kifungu cha  71(4) Mwajiri yoyote atakayeshindwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi atashitakiwa Mahakamani na akikutwa na hatia adhabu yake ni faini isiyozidi TSh.50,000,000 au kifungo cha miaka mitano au vyote kwa pamoja.

Pamoja na hayo, Mavunde amemuagiza Afisa Kazi Mfawidhi wa Mwanza kuwapa waajiri hao Amri tekelezi ya siku 30 kutekeleza matakwa ya Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Na. 6/2004 kwa kuwapa Wafanyakazi wao mikataba,malipo ya mshahara kwa kima cha chini cha sekta husika na kuwasilisha michango ya wafanyakazi katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top