Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Hii ndiyo huduma ya kwanza kwa mtu aliyegongwa na Nyoka

Huduma ya kwanza ni matibabu ya awali anayopata mgonjwa mara tu au muda mfupi baada ya kugongwa na nyoka kabla hajafikishwa kwenye kituo cha afya. Inaweza kufanywa na muathirika mwenyewe au mtu yeyote mwenye ujuzi wa kutoa huduma ya kwanza aliyepo karibu.

Malengo ya huduma ya kwanza
  • Kujaribu kuzuia kusambaa kwa sumu
  • Kulinda uhai na kuzuia madhara kabla mgonjwa hajapata matibabu
  • Kudhibiti dalili hatarishi za sumu
  • Kuandaa usafiri wa kumpeleka mgonjwa kwenye kituo cha tiba
  • Muhimu zaidi, Ni kuepuka kusababisha madhara zaidi.


Hatua za Huduma ya Kwanza
1. Mtie moyo mgonjwa (mara nyingi anakuwa na hofu).

2. Mlaze mgonjwa katika hali ya utilivu, hakikisha viungo havichezi . Viungo vikicheza huchangia sumu kusambaa mwilini.

3. Epuka kugusa sehemu iliyogongwa. Unapogusa sehemu iliyogongwa unasababisha sumu kusambaa kwa urahisi, kuingiza vimelea vya bakteria na damu kuvuja.

KUMBUKA : Iwapo nyoka ameuwawa unaweza kwenda nae katika kituo cha afya.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top