Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Jokate Mwegelo afunguka mazito baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya


Ikiwa ni siku moja imepita tangu Mwanamitindo na Mjasiriamali, Jokate Mwegelo ateuliwe na Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Hatimaye mwenyewe amefunguka jinsi alivyohaha hadi kupata nafasi hiyo.

Jokate amesema mwaka jana alitaka kukata tamaa kwenye maisha yake ya siasa kwani aliona giza mbele yake lakini hakufanya hivyo hii ni kutokana na kupokea maoni mengi kutoka kwa vijana ambao alikuwa anawashawishi kuingia kwenye siasa.

Akifunguka kuhusu Changamoto, Jokate amesema kuwa vijana wengi sio wavumilivu pale wanapopatwa na changamoto na ndio maana unakuta wanakata tamaa lakini wakati mzuri wa kuweza kujitathmini ni pale unapopatwa na changamoto.

==>Soma zaidi taarifa aliyoitoa Jokate Mwegelo kwa mashabiki wake

"Amini Mungu ni mwingi wa rehema kamwe hamtupi amtumainiye yeye!! Ahsante Mungu Wangu. Labda ni-share kitu kidogo, kuna muda mwaka jana mwishoni nilikuwa so down nilitamani kukata tamaa na kila kitu kwenye maisha nilikuwa pia sijaelewa vizuri hatma yangu kwenye siasa. Nilikuwa kwenye mkutano mkuu wa chama kuna mdada mmoja kutoka Arusha akanikimbilia na kunikumbatia kwa nguvu sana alikuwa na mama mmoja hivi walikuwa wamekuja kupiga picha namimi.

"Huyo dada mdogo hivi akasema ananipenda sana sana na mimi ndio nilimfanya aingie kwenye siasa na akagombea nafasi kupitia mkoa wa Arusha akashinda!! Nikabaki natabasamu. Ikanipa nguvu kubwa ya kupiga moyo konde na kusonga mbele. Nilifurahi kuona kuna mdada nimeweza kumhamasisha na kumpa ujasiri wa kugombea. Unaweza ukawa unapitia mitihani migumu sana kwenye maisha yako lakini inakubidi usikate tamaa saa zingine kwasababu tu ya wale wanaokutegemea, wanaokuangalia na kuvutiwa nawe na kujifunza kupitia maisha yako.

"Lakini zaidi kwasababu safari ya mafanikio ina milima na mabonde, inabidi upambane na kiukweli hakuna mafanikio yasiokuwa na changamoto. Na kuna muda changamoto ndio haswa zinatengeneza “character” zetu.
 
"Kikubwa zaidi wakati wa changamoto tukumbuke kuwa wanyenyekevu, wenye kujishusha na kumuomba Mungu aendelee kutupa imani, hekima na busara ya kusubiri wakati wake. Tukumbuke Mungu hamtupi mja wake. Nawatakia Jumapili Njema. Nawapenda Sana. Ahsanteni 🙏🏽"

Jokate kabla ya kuteuliwa jana alikuwa ni kada wa CCM ambapo kipindi cha nyuma alishawahi kuwa Kaimu Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi  (UVCCM) .
Download Our App

1 comments:

Nilichanganyikiwa na kuhuzunika mume wangu alipoomba talaka. Kisha nikawasiliana na Dk DAWN, baada ya kuona ushuhuda mwingi wa jinsi Dk DAWN alivyosaidia watu wengi kurejesha amani katika ndoa na uhusiano wao,
Pia niliona jinsi alivyotibu magonjwa mbalimbali na kusaidia watu wachache kutibu ugumba, niliamua kuwasiliana naye kwa msaada,
Aliahidi kusaidia wakati baada ya kumueleza kila kitu, nilimpa kila alichouliza na akafanya kazi yake, sasa mume wangu ananipenda sana na ananitendea kwa Matunzo. Nyumba yangu ni ya amani na imejaa furaha, shukrani zote kwa Dk DAWN,

Wasiliana naye ikiwa una tatizo lolote kwa sasa. Yeye ni WhatsApp: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com

Reply

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top