Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kamishna Jenerali Jeshi La Magereza Afanya Mabadiliko Ya Kiungozi Kwa Wakuu Wa Mikoa Na Vituo


Kamishna Jenerali wa Jeshi  la Magereza nchini, Phaustine Martin Kasike (pichani)  amefanya mabadiliko madogo ya kiuongozi kwa Wakuu wa Magereza wa Mikoa na Vituo vingine vya Magereza nchini.

Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Naibu Kamishna wa Magereza(DCP), Julius Sang’udi amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza kuwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wafungwa na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza(SACP), Salum Hussein.

Aliyekuwa Mkuu wa Gereza Mtego wa Simba, Kamishna Msaidizi wa Magereza(ACP), Msepwa Omary amehamishiwa Magereza Mkoa wa Singida kuwa Kaimu Mkuu wa Magereza mkoa huo na nafasi yake inakaimiwa na Mrakibu wa Magereza, Muta Tibalinda.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza (DCP), John Masunga amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza kuwa Mkuu wa Kitengo cha Viwanda vya Jeshi la Magereza, na nafasi yake imekaimishwa kwa aliyekuwa Mnadhimu wa Magereza Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi wa Magereza(ACP), Emmanuel Lwinga.

Wengine ni aliyekuwa Boharia Mkuu wa Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza (DCP), Afwilile Mwakijungu amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza kuwa Mdhibiti Mkuu wa Shirika la Magereza na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi wa Magereza(ACP), Goleha Masunzu. Pia aliyekuwa Afisa Mwandamizi sehemu ya Utawala Magereza Mkoani Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP), Benezeth Bisibe anakwenda kuwa Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mara.

Aliyekuwa Naibu Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri, Kamishna Msaidizi wa Magereza(ACP), Joel Matani anakuwa Mkuu wa chuo hicho na nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP), Wilington Kahumuza ambaye alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo hicho akishughulikia Manunuzi, Fedha na Utawala na nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Mwandamizi wa Magereza(SSP), Ahmad Seleman.

Wakati huo huo, Kamishna Jenerali wa Magereza amemteua Mrakibu wa Magereza (SP), Amina Kavirondo kuwa Msemaji Mkuu wa Jeshi la Magereza. Mabadiliko haya yanalenga kuboresha utendaji kazi ndani ya Jeshi la Magereza ili kuongeza ufanisi.

Imesainiwa na;
Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje – Ofisa Habari,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM,
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top