Na Khadija Seif,Globu ya jamii
JESHI la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) limesema litatoa huduma ya kupima afya za wananchi bure katika mikoa mbalimbali ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam.
Wakati Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo atatembelea wagonjwa katika Hospitali Kuu ya jeshi Lugalo.Akizungumza Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa jeshi hilo Kanali Ramadhani Dogoli amesema huduma hiyo itatolewa huduma hiyo Julai 25 mwaka huu.
Amesema Julai 25 ya kila mwaka huadhmishwa Siku ya Mashujaa wetu na hivyo watatumia siku hiyo kushiriki kwenye shughuli za kijamii.Amesema kuwa Makao Makuu ya JWTZ(Ngome) watakuwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Saalam.
"Wanachi wananchi watakaofika viwanjani hapo watapata fursa ya kupima shinikizo la damu ,kisukari ,uchunguzi wa kinywa na meno, uzito, kupima VVU kwa hiyari pamoja na kutoa ushauri nasaha.Upimaji huo utaanza saa moja asubuhi."Kila mwaka inapofika Julai 25 huwa inaadhiishwa siku ya mashujaa.Kwa JWTZ pamoja na mambo mengine huwa tunaadhmisha siku hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii,"amesema.
Pia JWTZ watafanya usafi katika maeneo mbalimbali na kwamba mbali ya Dar es Salam wanajeshi walioko mkoani Mbeya, Tabora na Pwani nao watashiriki kwenye shughuli za kijamii.Ameongeza kwa Dar es Salam JWTZ watafanya usafi katika katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke, hospitali ya Mbagala Zakhiem, hospitali ya Dar group na stendi ya mabasi ya Mbagala na Temeke.
Pia soko la Mbagala ,Temeke,Tandika na kutakuwa na upandaji wa miti katika shule ya Wailes.Ameeleza kwa upande wa Kamandi ya jeshi la nchi kavu Msangani amesema watatoa huduma ya vipimo kuanzia saa mbili asubuhi katika Hospitali ya Galagaza na kutoa misaada katika kituo cha watoto yatima Mwanalugali kilichopo Msangani.
Amesema kwa upande wa Kamandi ya jeshi la Anga itafanya usafi katika Shule ya Msingi ya Changanyikeni na Jeshi la Kamandi ya jeshi la wanamaji watafanya usafi katika Hospitali ya Vijibweni, Hospitali ya Kigamboni na soko kuu la Kigamboni.
Dogoli amesema Brigedi ya Nyuki Zanzibar itafanya usafi soko la Mombasa ,Sebuleni Majumba ya Wazee na Soko la Mwanakwerekwe.Wakati Brigedi ya Faru Tabora itafanya usafi katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Manyara.
Post a Comment