Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai, 2018 umepungua hadi kufikia asilimia 3.3 ikilinganishwa na asilimia 3.4 mwezi Juni, 2018.
Hayo yameelezwa jana na Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa sensa na Takwimu za Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ephraim Kwesigabo alipokuwa akitoa taarifa ya mfumuko wa bei kwa mwezi Julai mwaka huu.
Kwesigabo alisema, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2018.
“Kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 kumechangiwa hasa na kupungua kwa mfumuko wa bei wa baadhi ya bidhaa za vyakula, ambapo bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei kati ya Julai, 2017 na Julai 2018 ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 9.5, mtama kwa asilimia 17.8, unga wa mihogo kwa asilimia 14.1, matunda jamii ya machungwa kwa asilimia 22.2, maharagwe kwa asilimia 5.8 na mihogo mibichi kwa asilimia 12.5,” alifafanua Kwesigabo.
Aliendelea kusema kuwa ni zaidi ya miaka 15 tangu itokee tarakimu kama hiyo ya mfumuko wa bei ambayo iko vizuri kwa uchumi wa nchi.
Aidha alitaja hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki kama ifuatavyo; Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 umeongezeka hadi asilimia 3.1 kutoka asilimia 2.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018. Kwa upande wa Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 umeongezeka hadi asilimia 4.35 kutoka asilimia kutoka asilimia 4.28 kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2018.
Mfumuko wa bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.
2 comments
The latest casino, new and best slots and bonuses - DrmCD
ReplyNew casinos are here to help 포항 출장마사지 you 경상북도 출장안마 out at the 안성 출장마사지 most popular online slots and 문경 출장안마 casino games. We look forward to you joining with DrmCD 익산 출장안마 to discover how
Nilichanganyikiwa na kuhuzunika mume wangu alipoomba talaka. Kisha nikawasiliana na Dk DAWN, baada ya kuona ushuhuda mwingi wa jinsi Dk DAWN alivyosaidia watu wengi kurejesha amani katika ndoa na uhusiano wao,
ReplyPia niliona jinsi alivyotibu magonjwa mbalimbali na kusaidia watu wachache kutibu ugumba, niliamua kuwasiliana naye kwa msaada,
Aliahidi kusaidia wakati baada ya kumueleza kila kitu, nilimpa kila alichouliza na akafanya kazi yake, sasa mume wangu ananipenda sana na ananitendea kwa Matunzo. Nyumba yangu ni ya amani na imejaa furaha, shukrani zote kwa Dk DAWN,
Wasiliana naye ikiwa una tatizo lolote kwa sasa. Yeye ni WhatsApp: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
Post a Comment