UNAUKUMBUKA ULE WIMBO WA MWENGE WA UHURU?
Mwenge wa Uhuru
Na Emmanuel J. Shilatu
Hii ni kwa Wadau wa libeneke hili ambao wanashuhudia Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa na hawajui sababu zake, Inawezekana kabisa umeusahau ule wimbo wa Mwenge wa Uhuru ama haujawahi kuusikia kabisa wimbo huu mtaamu wa Mwenge wa Uhuru. Haya hapa ni baadhi tu ya mashairi ya wimbo huo uliokuwa maarufu sana enzi za Mwaalimu na sababu za uwepo wake
"Sisi tunataka kuwasha Mwenge
Tunataka kuwasha Mwenge
Na
kuuweka juu ya mlima ooo
Mlima Kilimanjaro.
Kuwasha
Mwenge
Kuwasha Mwenge
Na kuuweka
Kilimanjaro
Umlike hata nje ya mipaka yetu uletee
tumaini
Upendo mahali ambapo pana chuki
Heshima ambapo
pamejaa dharau
Matumaini na kadhalika
Haki penye
dhuluma
Maadili penye madili "
Kwa ubora wa mashairi yake na utam wa tenzi zake, nyimbo kama hizi zilisaidia sana kuwajengea Watu uzalendo kwa Taifa letu ambao uzalendo huo umeota mbawa. Kuna haja kubwa sana za kuzirudisha nyimbo zilizokuwa zikiimbwa miaka ya nyuma, zisizo na mfungamano wa kiitikadi!
Loading...
Post a Comment