Timu zikiingia uwanjani kuanzaq mpambano huo.
Mashabiki wa Azam waliochanganyika na wa Simba, wakiwa wamebeba Jeneza kuwakejeli mashabiki wa Yanga, kabla ya kuanza kwa mchezo huo.lakini hadi mwisho wa mchezo huo Jeneza hilo halikujulikana lilikopitia
Kasuku nao walikuwapo kushuhudia mtanange huo huku wakiwa na rangi ya Yanga na Bendera ya Yanga.
Mashabiki wa Azam wakiwa Tuliiiiii, wakiwa kama wamemwagiwa maji baada ya timu yao kupokea kichapo kitakatifu jioni ya leo.
Kiiza akiserebuka na Niyonzima kushoto...nyuma yao ni Bahanuzi |
Mashabiki wa Yanga, wakishangilia bao la kwanza.
BAO LA PILI; Wachezaji wa Yanga wakiwa wamemlalia Said Bahanuzi 'Spider Man' baada ya kufunga la pili |
Said Bahanuz, akishangilia mbele ya mashabiki wake baada ya mchezo huo kumalizika.
Mashabiki wa Yanga....... Ebwana eeeeh!!!! ushindi mtamu bwanaaaaaa!!!!
Wachezaji wa Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakishangilia ubingwa wao wakiwa na Kombe la Kagame baada ya kukabidhiwa rasmi walipoibanjua timu ya Azam Fc kwa mabao 2-0, katika mchezo wa Fainali uliozikutanisha timu hizo katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa leo jioni.
Post a Comment