Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HATIMAYE DK. SLAA ASALIMU AMRI

  •  AJIPELEKA POLISI KUHOJIWA KUHUSU MADAI YA NJAMA ZA BAADHI YA VIONGOZI WA CHADEMA KUUAWA

Katibu Mkuu wa Chadema, Wilbrod Salaa akiwasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mjini Dar es Salaam, kutii amri ya polisi iliyomtaka kutoa maelezo kuhusu madai yaliyotolewa na chama hicho juzi kati kwamba kuna njama zinafanywa na vyombo vya ulizni na usalama vya serikali kuwaua baadhi ya viongozi wa chama hicho. Kulia ni aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini,
Haya piteni hapa, Polisi akiwaonyesha njia Dk. Slaa na mwenzake

Baadhi ya watu waliokuwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kutaka kujua kilichokuwa kikiendelea
Hamjambo? Dk. Slaaa akasalimia baadhi ya watu waliokuwa eneo hilo
Kisha akazungumza na waandishi wa habari baada ya kuhojiwa na polisi

Na Bashir Nkoromo

Baada ya kujaribu kuweka kigingi kwamba Chadema hawatakwenda polisi kueleza kuhusu madai yao ya viongozi wa chama hicho kuundiwa njama za kuuawa na serikali, hatimaye leo, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Wilblod Slaa amejisalimisha makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam.
Dk. Slaa akifuatana na baadhi ya viongozi wa Chadema akiwemo mbunge wa zamani wa Arusha mjini Godbless Lema, alifika mida ya saa nne asubuhi kwa shangingi lake lenye namba za usajili T 875 AKS aina ya Toyota Landcruise.
Baada ya kufika Dk. Slaa, Lema na wakili Dk. Rugemereza Nshala, walishuka na kwenda kwa wenyeji wao Polisi tayari kwa kuhojiwa.
"Tumefika kuitika wito wa polisi" alisema Lema baada ya baadhi ya waandishi wa habari kuuliza nini kimewalazimu kuja polisi ilihali walikuwa wameshasema kwamba hawana imani na polisi?
“Tumepata wito na tumeitikia tambueni mjumbe hauawi sasa ni wito wa namna gani ngoja tukawasikilize lakini na ninyi waandishi wa habari hampitwi na kitu kila sehemu mpo” Dk Slaa akaongeza huku akicheka.
Baada ya kufika mapokezi Dk Slaa na Lema walielekezwa kwenda chumba namba 703 ambapo walikaa kwa muda wa dakika tano na kisha wakatoka kuelekea chumba namba 808 huku ofisa wa Polisi aliyevaa kiraia akiwataka waandishi wa habari wasiwafuate.
Katika Chumba namba 808 walichoingia ofisa huyo wa Polisi aliwakaribisha huku akisikia kuwaambia Dk Slaa,Lema na wakili wao Dk. Nshala kuwa wakaribie ingawa eneo hilo lipo, katika ukarabati na kisha kufunga mlango.
Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa jeshi la polisi Advera Senso, alisema Dk Slaa na wenzake waliitwa kwa ajili ya maelezo ya awali ya kusaidia uchunguzi dhidi ya malalamiko yao ya kuuawa.
Alisema jeshi la polisi limefungua jalada la uchunguzi na kwamba mlalamikaji ni ni lazima atoe maelezo yatakayoweza kufanyika kwa uchunguzi huo kabala ya jalada kupelekwa kwa Mwendesha mashtaka.
“Tumewaita kwa hati maalum, dhidi ya malalamiko yao naamini tutashirikiana nao kubaini ukweli na kisha tutafanyia kazi kwa kuwa wajibu wetu ni kumlinda kila mmoja hata kama atakuwa ametolea malalamiko yake chumbani”alisema Senso.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka Dk Slaa alisema suala aliloitiwa ni juu ya malalamiko yao ya kutishiwa kudhuriwa na kwamba alichowaeleza polisi ni kwamba wanapaswa kuyatolea kwanza maelezo ya taarifa za nyuma za kutishiwa kwao ikiwamo suala zima la kuwekewa vinasa sauti wakati akiwa mbunge mjini Dodoma.
Kila kitu kipo wazi nimewaambia kwa sasa sina maelezo mengine zaidi ya yale niliyotoa katika mkutano na waandishi wa habari, na kubwa nikawataka wanipe mrejesho wa taarifa mbali mbali za kutishiwa kwetu tulizowafikishia kabla”alisema Dk Slaa.
Wakili aliyefuatana na viongozi hao Dk. Rugemereza Nshala, alisema wateja wake wameahidi kupeleka maelezo waliyotoa mbele ya waandishi wa habari na kwamba suala la kuhojiwa ni la kisheria hivyo wananchi wasubiri kujua kitu gani kitaendelea.
Jumapili ya wiki iliyopita Dk Slaa akiwa na viongozi wengine wakuu wa Chadema,walidai kubaini mkakati wa makusudi wa kuwadhuru viongozi wakuu wa chama hicho, mpango waliosema unaratibiwa na baadhi ya vigogo katika idara ya usalama wa Taifa.




 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top