Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi-Zanzibar
Jeshi la Polisi Zanzibar linawashikilia wafanyakazi sita wa meli ya MV Skagit akiwemo mmiliki wake Bw. Said
Abdulrahman pamoja na Nahodha wa meli hiyo Bw. Mussa Makame Mussa na wanahojiwa kufuatia tukio la ajali ya meli hiyo
iliyosababisha vifo vya baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Bandari ya
Zanzibar.
Watuhumiwa hao walikuwa wakihojiwa katika Ofisi za Upelelezi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mjini Zanzibar
ambapo Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, ACP Yusuph Ilembo, amesema watuhumiwa hao wawataweza kufikishwa
ambapo Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, ACP Yusuph Ilembo, amesema watuhumiwa hao wawataweza kufikishwa
mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
Kamanda Ilembo amesema kuwa Makachero wa Jeshi la Polisi wanaendelea na uchunguzi na kutafuta taarifa nyingine
zinazohusiana na tukio hilo.
Hata hivyo, Nahodha wa zamu siku ya tukio hilo la kupinduka na kuzama kwa meli hiyo ya MV Skagit, Bw.Mussa Makame
Hata hivyo, Nahodha wa zamu siku ya tukio hilo la kupinduka na kuzama kwa meli hiyo ya MV Skagit, Bw.Mussa Makame
Mussa, ameelezea kwa ufupi jinsi ajali hiyo ilivyotokea na namna yeye alivyonusurika katika ajali hiyo.
Amesema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya kupigwa na dharuba na mawimbi yaliyoambatana na upepo mkali, ambapo yeye
alinusurika kufa maji baada ya kuruka kwa kutumia mlango wa mbele wa meli hiyo na kuanza kuogelea ambapo
alijichanganya pamoja na na abiria wengine walionusurika na kuokolewa na vyombo vya uokozi.
Wakati huo huo, Wapiga mbizi wa Vikosi vya Ulinzi na usalama leo wamefanikiwa kuzupata maiti ngingine za watu watano
Wakati huo huo, Wapiga mbizi wa Vikosi vya Ulinzi na usalama leo wamefanikiwa kuzupata maiti ngingine za watu watano
akiwemo mwanamke mmoja na wanaume wanne.
Katika upekuzi wa maiti hizo, Makachero wa Polisi walibaini kitambulicho cha kupigia kura kutoka kwa mmoja ya mwili
wa marehemu kitambulicho kilichokuwa na jina la Philip John Busiya aliyezaliwaq mwaka 1977 katika kijiji cha
Mapilinga kilichopo katika Kata ya Igokelo wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.Kupatikana kwa miili hiyo mitano, kunaifanya idadi ya maiti kufikia 73. Maiti nyingine 68 zilipatikana siku za
mwanzo baada ya kutokea kwa ajali hiyo ambapo kati ya hizo, maiti 54 zilitambuliwa na kuchukuliwa na ndugu na jamaa
kwa ajili ya mazishi.
Idadi ya miili ya watu waliopoteza maisha katika boti ya MV Skagit, imeongezeka kutoka 68 na kufikia 73, baada ya
vikosi vya uokozi, kufanikiwa kuopoa miili ya watu watanao, katika eneo la tukio karibu na kisiwa kidogo cha Chumbe,
kilichopo pembezoni mwa mji wa Zanzibar.
Maiti hiyo iliyopewa namba 72, pamoja na maiti nyingine nne, zimezikwa katika makaburi ya pamoja ya Kama yaliyopo
nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Eneo hilo la Kama pia lilitumika kwa kuwazika watu wengine waliokosa ndugu wakati wa ajali ya meli ya Spice Islander
iliyotokea Septemba 9, mwakaja 2911.
Kupatikana kwa miili hiyo, kumetokana na juhudi zinazoendelea kwa kuvishirikisha vikosi vya ulinzi na usalama,
wazamiaji wa makampuni binafsi pamoja na Mamlaka ya Bandari Zanzibar wakati wakiwa katika harakati za kuitafuta
boti hiyo, ili kuweza kubaini kama kuna miili mingine iliyosalia kwenye Meli hiyo chini ya Bahari.
Aidha, juhudi za kutaka kuiibua Meli hiyo zinaendele ambapo wazamiaji wa JWTZ, Polisi, KMKM, JKU, Bandari na wale wa
Makampuni binafsi na wale wa kujitegemea wakiendelea na kazi ya kutafuta mahali ilipo meli hiyo ili kuona kama
wataweza kupata miili mingine iliyonasa kwenye vyumba vya meli hiyo ambayo imekokotwa na maji kutoka eneo ilipozama
meli hiyo.
Post a Comment