MRISHO NGASA
Klabu
ya Azam FC inapenda kutoa taarifa rasmi kuwa milango iko wazi kwa klabu
yoyote kumnunu mchezaji MrishoNgassa kwa gharama ya $ 50,0000.
Azam
FC imefikia hatua hiyo baada ya mchezaji huyo kuonyesha kutokuwa na
mapenzi na klabu hiyo na badala yakekuipenda klabu aliyotoka ya Yanga.
Hivyo uongozi wa klabu unapokea maombi kwa klabu yoyote inayomuhitaji mchezaji huyo.
Azam
FC ilitoa nafasi ya upendeleo kwa klabu ya Yanga lakini hakuna ofa
iliyoletwa kuhusu, klabu imepokea ofakutoka Simba kumuhitaji mchezaji
huyo.
Ngassa
anauzwa siku chache baada ya kukubali kuvaa jezi ya Yanga na kuibusu
logo ya timu hiyo, baada yakumalizika kwa mchezo wa nusu fainali kati ya
Azam FC na AS Vita Club ya Congo DRC katika mashindano yaKombe la
Kagame yaliyomalizika Julai 28 mwaka huu.
SOURCE:http://www.azamfc.co.tz
Post a Comment