Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Balozi Tuvako Manongi kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja
wa Mataifa, New York.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano,
Julai 25, 2012 na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Peniel Lyimo kupitia
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo
ulianza jana, Julai 24, 2012.
Kabla ya uteuzi wake, Balozi Manongi
ambaye ni ofisa wa miaka mingi wa masuala ya nchi za nje, alikuwa Mshauri
Mwandamizi katika Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, New
York.
Balozi Manongi anachukua nafasi ya
Balozi Ombeni Y. Sefue ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Desemba 30,
mwaka jana, 2011.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
25 Julai,
2012
Post a Comment