Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anna Makinda, amevunja rasmi kamati ya Bunge ya Nishati na Madini baada ya wajumbe wa kamati hiyo kutuhumiwa kuhusika na rushwa katika tenda mbalimbali za shirika la umeme nchini TANESCO.
Katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini uliofanyika mwisho wa wiki hii huko mjini Dodoma, kuliibuliwa mambo mengi yenye kufedhehesha kuhusu TANESCO, ikiwa ni pamoja na madai ya baadhi ya wabunge kutajwa kuwa wamekuwa wakihusika na tenda haramu za kuuza vitu kadhaa katika shirika hilo, huku pia wakitajwa kuwa wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa mgao wa mara kwa mara wa umeme nchini, huku hali ya uzalishaji ikiwa sio mbaya kama inavyodhaniwa.
Post a Comment