Mkurugenzi wa masoko
na matukio wa TFF Jimmy Kabwe akisaini mkataba wa makubaliano ya udhamini wa
michuano ya Banc ABC SUP8R Soccer Tournament 2012 inayodhaminiwa na banc
ABCkulia kwake ni katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah, Mkurugenzi Mkuu wa benki
hiyo Boni Nyoni na Mkuu wa Idara ya fedha ya benki hiyo, Mwalimu
Zubery.
Osiah
akibadilishana hati na Nyoni
Benki ya ABC imesaini mkataba
wa miaka mitatu na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kudhamini
michuano ya BancABC Super 8 inayoshirikisha timu nane, nne kutoka Tanzania Bara
na nyingine nne kutoka Zanzibar.
Hafla ya utiaji saini
imefanyika leo (Julai 26 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam ambapo
Katibu Mkuu Angetile Osiah amesaini kwa niaba ya shirikisho wakati kwa upande wa
ABC, saini yake iliwekwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo kwa Tanzania,
Boniface Nyoni.
Mashindano hayo yataanza
Agosti 4-18 mwaka huu yakichezwa katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na
Zanzibar ambapo timu zote shiriki zitacheza katika vituo hivyo.
Uzinduzi rasmi wa mashindano
hayo utafanywa Agosti 2 mwaka huu na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki ya ABC
yenye makao yake makuu nchini Botswana, na ina matawi katika nchi za Msumbiji,
Zambia, Tanzania, Zimbabwe.
Katika uzinduzi huo, CEO
ataelezea thamani ya mkataba huo ambapo utahusisha gharama za malazi, usafiri,
vifaa na uendeshaji wa mashindano hayo.
Akizungumza baada ya kutia
saini, Osiah amesema hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya TFF kuwa na mashindano
mengi yatakayosaidia kuziandaa timu kabla ya kuanza Ligi Kuu.
Naye Nyoni amesema ABC
imekubali kuingia kudhamini mpira wa miguu ikiwa ni lengo la kuchangia ustawi wa
mchezo huo na kutoa sehemu ya faida wanayopata kwa kupitia michezo.
Timu zitakazoshiriki
mashindano hayo ni zile zilizoshika nafasi tatu za juu katika Ligi Kuu ya
Tanzania Bara na Ligi Kuu ya Zanzibar. Nyingine ni timu iliyoshika nafasi ya
kwanza kwenye Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara na Ligi Daraja la Kwanza ya
Zanzibar ambazo nazo kwa kushika nafasi hizo zimeshaingia katika Ligi
Kuu.
chanzo: Bongostaz & FrancisGodwin Blogs
Post a Comment