Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Tuipitishe hii sheria kwenye Katiba yetu ya nchi?


PICHANI: Jinsi mwanamke huyo alivyouawa. Tukio zima lilianzia kushoto juu kwenda kulia.
Ameuawa kwa kupigwa risasi kwa bunduki aina ya AK47 huku wanakijiji waliokusanyika eneo hilo wakifurahia kwa namna ya kupendeza, hili ni tukio ya kushitusha pale mwanamke alipouawa nchini Afghanistan ndani ya ngome ya mpenzi wake wa Taliban.
Mwanamke huyo mwenye miaka 22 ambaye inasemekana aliolewa na mfuasi wa kundi la kijeshi la Taliban, alipigwa risasi na kufa kwa tuhuma za kutembea na kamanda wa kundi la Taliban.
Picha za kuogofya zinaonesha kundi la wanaume wa miraba minne wakiwa wameungana kushuhudia askari wenye bunduki wakimmiminia risasi kichwani na mgongoni wakati wa mauaji hayo kijiji cha Qimchok, kwenye Jimbo la Parwan nchini Afghanistan.
Mfululizo wa picha zenye ubora hafifu za mauaji hayo ya kikatili zinamuonesha mwanamke, anayefahamika kama Najiba, akianguka sakafuni, huku kundi la wanaume walioko kwenye mwinuko ulioko jirani wakishangilia kwa kusema, "Mungu ni Mkubwa!"
Mlenga shabaha asiyefahamika, ambaye anaonekana akiwa kavalia kofia ya rangi ya machungwa, akimuua kwa urahisi, huku akiendelea kuufyatulia risasi mwili wake hata baada ya kufa na kuukaribia zaidi.
Maofisa nchini Afghanistan walisema mauaji hayo yamekuja kufuatia ugomvi kati ya wafuasi wawili wa Taliban, ambao walizozana kuhusu mwanamke huyo.
Gavana wa Jimbo la Parwan Abdul Basir Salangi alisema kwamba watu wote wa Taliban 'walikuwa na mahusiano fulani na mwanamke huyo', badala yake wakaamua kumtia hatiani kwa kufanya ngono 'kujiepusha na aibu'.
Picha za kuhuzunisha zimepatikana kutoka kwenye video ambayo haikuelezwa ilirekodiwa lini, licha ya kwamba inadhaniwa kuwa mauaji hayo yalifanyika wakati fulani mwishoni mwa mwezi Juni.
Video hiyo ilikabidhiwa na mwanakijiji wa Qol kwa Serikali ya Jimbo la Parwan, iliyoko kaskazini mwa mji wa Kabul, msemaji wao, Roshna Khalid ameeleza jana.
Hakuna dalili zozote za kama kuna chochote kilichoendelea kwa Kamanda wa Taliban ambaye anadaiwa kutembea na mwanamke huyo dhidi ya mume mtu.
Video hiyo imelaaniwa na Serikali ya Afghanistan kwamba ni kinyume cha Uislamu na si ubinadamu.
Mauaji ya wananchi wanaojihusisha na ngono yalishika chati wakati uongozi wa Taliban ulipokuwa madarakani.
Walishika hatamu za nchi kuanzia 1996 hadi 2001, pale walipong'olewa na Marekani waliovamia na kumuua Kiongozi wa kundi la Al Qaeda, Osama bin Laden baada ya mashambulizi ya Septemba 11. Swali la kujiuliza, hii sheria nasi tuiige? Ni wanawake wangapi wangepona?
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top