Klabu ya Arsenal imepokea maombi kutoka
vilabu viwili vikuu vya mji wa Manchester vikitaka kumsajili nahodha wa klabu
hiyo Robin van Persie pamoja na klabu ya Italia Juventus.
Mshambuliaji huyo
mwenye umri wa miaka 28 kutoka Uholanzi imearifiwa kuwa hatofuatana na kikosi
cha Gunners kinachosafiri kwenda Bara Asia kwa mechi tatu za kujipima
nguvu.
Imefahamika kuwa Man.city, United na Juventus zimewasilisha kiango kinachokaribia pauni milioni 15 za Uingereza ingawa Arsenal huenda isikubali ila kiasi kilicho kati ya pauni milioni 25 na 30.
Nahodha na mchezaji bora wa mwaka Van Persie alikataa kuanza majadiliano ya kuongezea mda wake wa kuichezea Arsenal punde baada ya mechi dhidi ya West Bromwich iliyomalizika kwa ushindi wa 3-2 na kuiweka Arsenal kwenye njia ya kushiriki Ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Huenda uwezekano wa kushiriki Ligi ya mabingwa ukawa chachu ya Van Persie kukubali kukaa pamoja na shughuli ya usajili wa washambuliaji wawili Lukas Podolski kutoka klabu ya FC Cologne kwa kitita cha pauni za Uingereza milioni £10.9m.
Arsenal ilitarajiwa kumuongezea malipo Mdachi huyo kwa kuandika mkataba wa miaka minne na kumridhisha yeye na familia yake wasiopenda kuhama kutoka London.
Mkataba wa Van Persie unamalizika mwaka 2013 na bado msimamo wake ni ule ule wa kutosaini mkataba mpya.
Mshambuliaji huyo
aliyejiunga na Arsenal kutoka klabu ya Feyenoord kwa malipo ya pauni milioni
£2.75 miaka minane iliyopita, ameweza kufunga jumla ya mabao 53 katika michezo
53 kwa klabu yake na Taifa katika kipindi cha msimu
uliopita.
Post a Comment