Na Kibada Kibada-Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe ameagiza kampuni ya utafiti na uchimbani madini ya Red O-Mining ltd kutoka China kusimamisha mara moja shughuli zote za utafiti kwa kuwa wamekiuka sheria za nchi kwa kufanya utafiti ndani ya pori la hifadhi ya wanyama la Rukwa Lukwati lililoko Hifadhi ya Taifa ya Katavi kinyume na sheria.
Mkuu huyo wa Mkoa alitoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa wawekezaji hao wanafanya shughuli za utafiti na uchimbaji wa Madini katika pori hilo la hifadhi kinyume na taratibu za kisheria za nchi pamoja na kuwa wanayo leseni ya kufanya utafiti inayowaruhusu waliyoipata kutoka wizara ya nishati na Madini lakini hawana kibali kinachowaruhusu kufanya utafiti ndani ya hifadhi.
Pamoja na kupata leseni hiyo walipatiwa barua kutoka wizara ya Maliasili na Utalii na idara ya mazingira inayowaelekeza kuwa wakifika eneo la kufanyia utafiti wawaone wamiliki wa eneo kupitia ofisi za wanyama pori wilaya husika,ya Mpanda lakini hawakufanya hivyo, badala yake waliamua kuingia katika pori hilo la hifadhi la Katavi na kuendelea na shughuli zao za kiutafiti bila kuwa na kibari cha kufanya shughuli hizo ndani ya hifadhi kwa kuwa ni kinyume na taratibu.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Josephine Rupia alipotakiwa kuelezea suala hilo mbele ya Mkuu wa Mkoa alieleza kuwa watafiti hao walifika ofini na kutoa kuomba wapatiwe eneo la kufanya utafiti ndani ya hifadhi ambapo aliweeleza kuwa hairuhusiwa kufanya shughuli hiyo ndani ya hifadhi hivyo wanatakiwa wawasiliane na wamiliki ambao ni Wahifadhi wa wanyama pori Rukwa Lukwati mapori yaliyoko ndani ya hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Kaimu Afisa Maliasili huyo alieleza kuwa hata kwa mjbu wa barua waliyopewa kutoka ofisi ya maliasili na mazingira inawaelekeza kuwa wafanye shughuli zao nje ya eneo la hifadhi ya wanyama na siyo ndani ya hifadhi wao walivunja sheria kwa kuwa wameingia kwa nguvu na hawajaruhusiwa.
Naye Afisa wanyapori wa Pori la Luafi na Rukwa Lukwati Zulu Ng’ondya alisema kuwa wawekezaji hao wamevuna sheria za nchi za kufanya utafiti ndani ya hifadhi ya wanyama sheria namba 5 ya mwaka 2009 kifungucha 20(1-3) Wawekezaji hao wanaofanya utafiti kwa ajli ya kuwekeza katika sekta ya madini wamevunja sheria ya nchi.
Meneja migodi Kanda ya magharibi Giliard Luyoka anasema ofisi yake iliwapokea wawekezaji hao na kumwonyesha liseni waliyopewa kutoka wizara ya Nishati na Madini ya kuwaruhusu kufanya utafiti wa madini nao wanatoa liseni tu bila kujali watafanyia utafiti eneo gani,hivyo kwa mantik hiyo kabla ya kufanya shughuli ni vyema taasisi zote zikashirikishwa katika maeneo ya kufanyia utafiti ili kuondoa migongano inayojitokeza kama livyo kwa wawekezaji hao.
Mmoja wa wawekezaji hao aliyejitambulisha kwa jina la Zhou Chaoxian, akiongea lugha ya kiingereza kwa shida kwa niaba ya wenzake waliojitambulisha kwa jina la Chang bao chen, Wud, Jie Wang, Wentao Yu, Du Wei pamoja na Xiaoxun Na, Kiongozi huyu alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa wao wanatumia ramani waliyopewa kuwa wako nje ya hifadhi pamoja na kuelezwa kuwa wako ndani ya hifadhi.
Hata hivyo baada ya kubanwa walikubali kuwa wamefanya makosa ingawa waliomba kupewa muda wa kuondoa vifaa vyao vya utafiti ndani ya Hifadhi wakati wakiendelea na taratibu nyingine kuweza kulipatia ufumbuzi suala hilo.
Kutokana na maelezo hayo Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliagiza kusimamisha mara moja kwa shughuli zote za uchimbaji na kufukishwa mahakani sheria ikuchukua mkondo wake na haki itendeke,pamoja na kuwa wawekezaj wanahitajika lakini wafanye kazi zao kwa kufuata utaratibu na sheria za nchi.
Pia ameagiza zana zote zilizoko eneo la kazi wanapofanyia utafiti kuziondoa na kusubiri taratibu za ksheria zikendelea.
chanzo: FullshangweBlog
Post a Comment