Warembo hao
wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao litakalo fanyika
kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hotel.
Warembo hao
wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao litakalofanyika kesho
kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hotel.
Warembo hao
wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao litakalofanyika kesho
kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hotel.
Warembo hao
wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kumaliza mazoezi yao.
*Mrembo wa Sinza kupatikana leo
Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya kumsaka mrembo bora waKitongoji cha
Sinza, Redds Miss Sinza 2012 yanafanyika leo kwenye ukumbi wa Mawela
Social Hall (Ten Star Lounge) uliopo karibu na hoteli ya Vatican
City.
Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 14
wanaowania taji la kituo hicho pamoja na kuiwakilisha kitongoji cha Sinza kwenye
mashindano ya Kanda ya Kinondoni na baadaye Miss
Tanzania.
Mbali ya taji (crown) na nafasi ya kuiwakilisha
Sinza katika Mashindano ya Kanda ya Kinondoni, pia mshindi wa kwanza katika
shindano hilo atajinyakulia kitita cha sh. 500,000/= katika mashindano hayo
yatakayopambwa na bendi ya African Stars “Twanga Pepeta International’ ambao
watakuwa wakitambulisha baadhi ya nyimbo zao mpya na Msanii wa vichekesho wa
kundi la Ze Comedy la Chanel 5, Masawe Mtata, atakayekuwa akitambulisha video na
wimbo wake mpya wa Uongo Kweli.
Akizungumza na mtandao huu, Mratibu wa mashindano
hayo kutoka kampuni ya Calapy Entertainment, Majuto Omary, alizitaja zawadi
nyingine kuwa ni shs 400,000 kwa mshindi wa pili, sh. 300,000 kwa mshindi wa
tatu . Mshindi wa nne na wa tano watapata sh. 150,000 kila mmoja na waliobaki
watapata sh. 100,000 kila mmoja kama kifuta jasho.
Aidha Majuto, aliongeza kuwa mbali ya kutembea
jukwaani kwa ‘catwalk’ kwa warembo hao, pia kutakuwa na shindano la kusaka
vipaji ambapo warembo watachuana ili kumpata Mafoto Miss Talent Sinza 2012,
ambapo mshindi atapata sh. 50,000 kutoka mtandao wa
sufianimafoto.blogspot.com.
“Maandalizi yamekamilika na viingilio vitakuwa ni
sh. 10,000 kwa viti vya kawaida na sh. 25,000 kwa vitu Maalum (VIP), tumeandaa
shoo fupi na ya aina yake ili baadaye mashabiki wa fani ya urembo wa kitongoji
cha Sinza wapate fursa ya kusugua kisigino na bendi ya Twanga Pepeta,” alisema
Majuto.
Majuto aliwataja Warembo wanaowania taji hilo kuwa
ni pamoja na Mariam Miraji, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Judith
Sangu, Eva Mushi, Vailet John na Esther Mussa.
Warembo wengine ni Christina Samwel, Nahma Said,
Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi, Brigitter Alfred na Merina
Mushi.
Shindano hilo limedhaminiwa na Redds Premium Cold,
Dodoma Wine, Gland Villa Hotel, Clouds FM, mtandao wa
sufianimafoto.blogspot.com, Brake Point, Fredito Entertainment, Screen
Masters, Lady Pepeta na flexi.
Post a Comment