Yanga
wakishangilia Kombe lao baada ya kukabidhiwa jioni
hii
Mashabiki wa timu ya Yanga wakishangilia mara baada ya timu yao kupata goli la kuongoza katika mchezo huo
|
Kikosi cha Yanga leo |
YANGA ya Dar
es Salaam imetwaa Kombe la Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe
la Kagame, jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, baada ya kuifunga Azam FC
mabao 2-0.
Yanga sasa
imebakiza mara moja kufikisha idadi sawa na wapinzani wao wa jadi, Simba kutwaa
Kombe hilo, mara tano kwa sita. Yanga ilibeba taji hilo 1975, 1993, 1999, 2011
na 2012.
Mashujaa wa
Yanga leo walikuwa Hamisi Kiiza aliyefunga bao la kwanza dakika ya 44 na Said
Bahanuzi aliyefunga la pili dakika ya tatu ya muda nyongeza, baada ya kutimu
dakika 90 za mechi hiyo.
Kiiza
alifunga bao lake, baada ya kuuwahi mpira uliookolewa na kipa Deo Munishi ‘Dida’
na kumpiga chenga kipa huyo kisha kuusukuma mpira nyavuni.
Bahanuzi
aliuwahi mpira mrefu uliopigwa na beki Oscar Joshua na kuwazidi ujanja mabeki wa
Azam kabla ya kumtungua Dida.
Mechi hiyo
imechezeshwa vema na refa Thierry Nkurunzinza kutoka Burundi, akisaidiwa na
Simba Honore wa Rwanda na Peter Sabatia wa Kenya, wakati mezani atakaa Issa
Kagabo wa Rwanda, Kamisaa Hassan Amir wa Somalia na Mtathmini wa marefa ni
Anangwe Robert wa Kenya.
Yanga SC;
Ally Mustafa ‘Barthez’, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Nadir Haroub
‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid Gumbo/Juma Seif
‘Kijiko’, Haruna Niyonzoma, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na David Luhende.
Azam FC; Deo
Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris,
Jabir Aziz, Kipre Tcheche/Mrisho Ngassa, Salum Abubakar, John Bocco ‘Adebayor’,
Ibrahim Mwaipopo na Ramadhan Chombo ‘Redondo’. Benchi; Mwadini
Ally, Samir Haji Nuhu, Joseph Owino, George Odhiambo, Mrisho Ngassa, Khamis Mcha
‘Vialli’ na Gaudence Mwaikimba.
Katika
mchezo uliotangulia wa kusaka mshindi wa tatu, AS ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) iliifunga APR ya Rwanda mabao 2-1, mabao yake yakifungwa na Magola
Mapanda dakika ya 18 na Mutombo Kazadi dakika ya 67, wakati la kufutia machozi
la timu ya jeshi la Rwanda, lilifungwa na Jean Mugiraneza dakika ya
89.
Post a Comment