Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manjikulia na Makamu mwenyekiti Clement Sanga wakati wa uchaguzi huo jana
Habari kwa hisani ya dinaismailblogspot.com
Yusuf Manji
amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa klabu ya Young Africans Sports
Club, uchaguzi ulioitishwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi, kufuatia
kujiuzuru kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji, mwenyekiti na
makamu wake.
Akitangaza
matokeo hayo, majira ya saa 10:30 alfajiri katika ukumbi wa Diamond
Jubilee, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Yanga Jaji John
Mkwawa amemtangza Manji kama mishindi wa nafasi ya uenyekiti kufuatia
kupata asilimia 97% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi hiyo.
Nafasi ya
Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Clement Sanga aliyejipatia asilimia 62%
ya kura zote zilizopigwa katika nafasi ya u makamu mwenyekiti.
Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda na George Manyama wamechaguliwa katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya Utendaji.
Jaji Mkwawa
amewashukuru wana Yanga kwa kuwa wastaarabu na watulivu, kitu
kilicholekea kufanyika uchaguzi kwa amani na zoezi hilo kumalizika
salama pasipo kuwa na rabsha yoyote.
Matokeo kamili ya wagombea ni:
Nafasi ya Mwenyekiti:
Yusuf Manji (kura 1876) 97.0%, John Jembele (kura 40) 2.6%, Edgar Chibura (kura 4) 0.24%
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:
Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%, Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%
Nafasi ya Ujumbe:
Abdallah Bin Kleb (kura 1942), Moses Katabaro (kura 1068), Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295), Graticius Ishengoma (kura 247), Jumanne Mwamenywa (kura 251), Justine Baruti (610), Lameck Nyambaya (kura 425), Omary Ndula (kura 170), Peter Haule (441), Ramadhan Said (249), Yono Kivela (123)
kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni
Mwenyekiti: Yusuf Manji,
Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga
Wajumbe: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge Manyama
Post a Comment