Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012,
kulikuwa na habari yenye kusomeka 'Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais
2015'. Habari hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala
umekuzwa zaidi baada ya Wabunge ndugu Halima Mdee na ndugu Joshua Nassari
kukanusha maneno waliyonukuliwa kusema. Napenda kusema masuala
yafuatayo.
Moja, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola, Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi. Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwemo Joseph Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamata na Peter Serukamba. Wabunge hawa hawakualikwa na mimi na wala sikufanya mazungumzo nao yeyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumza au hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa.
Waheshimiwa wote walipewa nafasi ya kusalimia na wote walizungumza. Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo ni ndugu Halima Mdee, Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.
Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya documentary ya tamasha lile la kihistoria.
Pili, sikuhusika kwa namna yeyote ile na kuandikwa kwa habari hii iliyozusha mjadala. Wala sikujua kama habari hii ingeandikwa maana katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja maana nilitaka liwe tukio la Kigoma tu.
Kama mwandishi kaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi itaonekana kwenye videos hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi zao nini walisema Kigoma na kipi kiliwasukuma kusema walioyasema Kigoma. Nisingependa kuhusishwa kwa njia yeyote ile na matamshi yao, habari iliyowanukuu na hata makanusho yao. Maana mwisho wa siku ukweli ndio utasimama.
Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya urais yanapotajwa zinashangaza sana.
Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Urais mpaka hapo mchakato utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.
Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema 'weka akiba' sio akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba ya maneno. Tusimalize yote.
Zitto

Mdee Naye amkana Zitto na Urais
Kwenye
barua yake kwenda kwa uongozi wa juu wa gazeti la mwananchi, hii ni sehemu ya
barua yake.
Nasikitika kutumia nafasi hii kukuandikia kukutaarifu kuwa gazeti lako la Mwananchi la Julai 23, 2012, katika habari yake iliyoongoza ukurasa wa kwanza (lead story) limenilisha maneno na kunikuu isivyo sahihi.
Katika habari hiyo yenye kichwa cha habari kisemacho “Wabunge wamsafishia Zitto njia ya urais 2015,” gazeti lako limeandika hivi “Mdee aliyepewa nafasi ya kuwasalimia wananchi alisema amekuwa na Zitto tangu Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kwamba kutokana na ujasiri na umahiri wake katika kutetea masilahi ya wanyonge na taifa, anafaa kuwa mmoja wa viongozi wa juu katika Taifa.”Gazeti lako pia katika aya iliyofuata limenukuu kuwa mimi nimesema;
*“Ndugu zangu watu wa Kigoma, kwa kweli mna bahati sana, achilia mbali kuwa na vipaji katika sanaa ya muziki na michezo hasa mpira wa miguu, lakini mna wanasiasa wakali ambao ni tishio hapa nchini. Mimi namkubali sana Zitto Kabwe na ninaamini kuna siku atakuwa kiongozi wa juu katika nchi yetu," alisema Mdee”
Nasikitika kusema kuwa gazeti lako limeandika habari zisizo za kweli kwa kunilisha *maneno na kudai kuwa mimi ndiye nimesema maneno hayo, kisha kuyaweka kwenye nukuu, likisema kuwa ni nukuu yangu. Sijajua nia au kusudio la gazeti lako kuamua kupotosha ukweli na kushindwa kabisa kuninukuu kwa usahihi, kama inavyotakiwa katika misingi ya taaluma ya habari.
Nasikitika pia kusema kuwa gazeti lako ambalo limeonekana kujijengea heshima miongoni mwa wasomaji wa kada mbalimbali nchini na hivyo linapaswa kuwa mfano wa kuigwa, linaweza kusigina misingi ya uandishi wa habari na hususan katika kufuata maadili ya taaluma hii muhimu, kwa kiwango cha kufanya moja ya dhambi kubwa ya kukilisha maneno chanzo cha habari.
Kwa ajili ya kutunza heshima ya gazeti lako, lakini pia kwa ajili ya maslahi mapana ya taaluma ya habari na jamii ya Watanzania, nakuandikia kulitaka gazeti lako likanushe maneno liliyoninukuu katika toleo hilo la Julai 23, 2012. Ni vyema sana hilo likafanyika kwa uzito unaostahili kama ilivyoandikwa katika toleo hilo.
Habari hiyo imeniletea usumbufu mkubwa hasa kwa wanachama wa chama changu, CHADEMA, ambao wanajua kuwa chama chao makini ni mahiri katika kufuata katiba, kanuni na taratibu katika kuendesha mambo yake kwa manufaa ya watu wote. Napenda kuwa mmoja wa Watanzania makini na viongozi wanaojua wajibu, ikiwemo kufanya nini na kusema nini, mahali gani na wakati gani.
Nakutakia utekelezaji mwema katika hilo.

Nassari naye amsaliti Zitto Kabwe
Katika
barua yake kwenda kwa mhariri mtendaji mkuu wa Mwananchi. Hii ni sehemu ya
waraka huo wa Nassari.
Nukuu hiyo si ya kweli. Nimesikitishwa sana na upotoshaji mkubwa wa kunilisha maneno mdomoni uliofanyika katika sehemu kubwa ya habari hiyo (mbali na nukuu hiyo) kwa maslahi ambayo sijui ni ya nani.
Wakati ukijiandaa kuchukua hatua kutokana na sababu ya pili ya kukuandikia barua hii ambayo nitaieleza punde hapa chini, naomba utafakari masuala kadhaa, ikiwemo; kwa nini ilichukua siku zaidi ya tano kwa habari hiyo kuandikwa?
Pili, kutokana na usumbufu mkubwa ambao nimeupata kutoka kwa Watanzania wa maeneo mbalimbali wanaotarajia kuniona mwakilishi wao nikizungumzia masuala yanayowahusu wao, ambayo ni muhimu zaidi kuliko jambo jingine lolote kwa sasa.
Lakini pia nikiwa Mtanzania anayetambua umuhimu na unyeti wa nafasi ya urais katika nchi hii na kwamba inaamuliwa kwa maslahi mapana ya umma wa Watanzania wala si uchu wa watu wachache, hivyo nisingeweza kutamka maneno hayo ambayo gazeti lako limeandika, naomba kukuandikia rasmi kukutaka ukanushe habari hiyo ukurasa wa mbele kwa uzito huo huo ulioipatia habari hiyo katika toleo tajwa.
Lakini pia nikiwa Mtanzania ambaye ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho kinaamini kuwa kwa sasa suala la urais si kipaumbele, bali muhimu kwa wakati huu ni kushughulika kujua mizizi au vyanzo vya matatizo makubwa yanayowakabili Watanzania ikiwemo umaskini, ujinga, maradhi, ufisadi na utawala mbovu wa CCM, kwani serikali imekuwa ikishughulikia matokeo.
Kama ambavyo chama changu, Watanzania wengine makini na mimi mwenyewe, naamini kuwa kwa sasa suala la muhimu kwetu kama taifa ni kutafuta mizizi au vyanzo vya matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ya Watanzania.
Kwa chama changu na mimi mwenyewe pia kama mwakilishi makini wa Watanzania, naamini kuwa siku zote suala la urais linategemea mahitaji ya Watanzania na kamwe haliwezi kuamriwa kwa kufuata matakwa na utashi au uchu wa watu binafsi.
Lakini pia suala la nikiwa kama mwanachama mwaminifu wa CHADEMA na ninayeipenda nchi yangu kwanza, naamini kuwa suala la urais linafuata katiba, kanuni na taratibu za chama, hatua ambayo haijafikiwa kwa sasa.
Naomba kusisitiza kuwa sijawahi kutamka, siwezi kutamka na sitarajii kutamka maneno hayo uliyoyaandika kwenye gazeti tena kwa kuninukuu na kuniwekea maneno mdomoni. Naomba kurudia tena kukutaka ukanushe habari hiyo ukurasa wa mbele kwa uzito huo huo ulioipatia habari hiyo katika toleo tajwa.

Chanzo: ChademaBlog
Post a Comment