Baadhi ya wananchi na maaskari wakijadiliana jambo kwenye mwili huo wa Afande Dunga. |
Nakala ya barua ya askari Dunga kwa Waziri wa Mambo ya Ndani. |
***************************************
Na Danstan Shekidele
Siku
chache kabla ya kifo chake askari polisi mwenye namba F 3276, Donald
Mathew (33), aliyejinyonga juu ya mti katika daraja la Shani, mkoani
Morogoro alimwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani kueleza
kinachodaiwa kuwa ni ufisadi unaofanywa na vigogo wa polisi nchini,
imebainika.
Polisi
huyo aliyefahamika sana kwa jina la Dunga aliwahi kutoa tuhuma nzito
dhidi ya maofisa, wakaguzi na polisi wa kawaida, mkoani Morogoro mwaka
jana lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya maofisa hao.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fustine Shilogile, jana alisema jeshi
hilo, lilipokea taarifa za kujinyonga Mathew jana asubuhi.
Alisema
askari huyo, aijinyonga kwa kutumia vipande vya kamba ya kanga ambavyo
viliunganishwa na hakuacha ujumbe wowote unaoeleza sababu ya kuchukua
uwamuzi huo.
Alisema askari huyo kabla ya kufanya tukio hilo, alionekana mitaani akinywa pombe katika Baa ya Shani.
Alisema
baada ya kuonekana amelewa, Mathew aliamua kuvua nguo zote na kubaki
mtupu, kitendo kilichofanya baadhi ya askari polisi waliokuwa eneo
hilo, kumfuata na kumsihi avae nguo.
Alisema marehemu, alihamishiwa mkoani Singida kikazi, lakini Novemba, mwaka jana aliamua kuacha jeshi.
“Pamoja
na kwamba marehemu aliacha kazi mwaka jana, sisi kama jeshi bado
tunamtambua kama askari mwenzetu… kwa msingi huo tutasafirisha mwili
wake Agosti 8, mwaka huu kwenda nyumbani kwake mkoani Kilimanjaro,”
alisema Kamanda Shilogile.
Alipoulizwa
kama kifo cha Mathew kimesababishwa na baadhi ya askari waliohusishwa
kwenye tuhuma za kuhusika na biashara za dawa za kulevya, Kamanda
Shilogile alisema uchunguzi unaendelea, na kwamba ikibainika kama kuna
askari aliyehusika atachukuliwa hatua kali.
Hata
hivyo, askari huyo mwishoni mwa mwaka jana, alitoa tuhuma mbalimbali
ambazo zilichapishwa katika moja ya magazeti linalotoka mara mbili kwa
wiki, zikiwatuhumu askari 9 wa kikosi cha kupambana na majambazi wa
kutumia silaha kupokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara wa dawa za
kulevya.
Tuhuma
nyingine alizotoa ni polisi kukamata majambazi wenye silaha, lakini
huachiwa baada ya kupewa fedha na mali mbalimbali, hivyo kushindwa
kuwafikisha kituoni.
Alisema
tuhuma nyingine ni polisi kuwakamata wafanyabiashara wa pombe haramu
aina ya gongo na bangi bila kuwachukulia hatua zozote baada ya
kuhongwa.
Tuhuma
nyingine, zinazodaiwa kufanywa na askari hao ni kushirikiana na
matapeli, kutapeli raia wa kigeni na kushirikiana na majambazi kuvunja
maduka na kuiba mali za wafanyabiashara nyakati za usiku.
Post a Comment