Sensa ya
watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kutambua na kusambaza takwimu za
kidemokrafia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao nchini katika kipindi
maalum.
Watu gani wanaostahili
kuhesabiwa wakati wa sensa ?
Wakati karani wa sensa atakapopita
kwenye kaya ( eneo amabalo watu kwa kawaida huishi na kula pamoja) atawahesabu watu
wote waliolala katika kaya husika usiku wa kuamkia siku ya sensa ni lazima
wahesabiwe. Usiku wa kuamkia siku ya sensa ni usiku wa siku ya Jumamosi, tarehe
25 Agosti 2012, kuamkia siku ya Jumapili tarehe 26 Agosti, 2012. Hii ina maana
kwamba wale wote waliolala katika kaya hiyo usiku wa kuamkia Jumapili ya tarehe
26Agosti, 2012 wahesabiwe kwenye kaya hiyo.
Kundi lingine litakalohesabiwa ni
wale wote ambao hawakulala katika kaya hiyo usiku huo wa kuamkia siku ya sensa
lakini walikuwa wamekwenda shamba kulima, kuvuna, kuwinda, machungani au wako
katika kazi za usiku na waliolala kwenye msiba wa jirani na kaya zao. Kundi
hili ni la wale ambao huwa wanarudi nyumbani asubuhi baada ya kazi za usiku.
Walio katika kaya za jumuiya ( kaya
za pamoja kama vile hoteli, magereza, mabweni,
hospitali) ambao walilala kwenye kaya hizo usiku wa kuamkia siku ya sensa.
Wageni, watumishi na watu wote wasio
na makazi maalum au wale wanaohamahama, ambao walilala nchini usiku wa kuamkia
siku ya sensa.
Watu wote ambao siyo raia lakini
wanaishi nchini na walilala nchini usiku wa kuamkia siku ya sensa. Kundi hili
pia litawahusha mabalozi wa nchi za nje watakaolala nchini usiku wa kuamkia
siku ya sensa, nao pia watahesabiwa.
Wasafiri ambao wako kwenye meli,
magari, ndege ,,,,ambao walikuwa nchini usiku wa kuamkia siku ya sensa bila
kujali kama vyombo hivyo ni vya hapa nchini
ama ni vya nje ya nchi.
Pia watoto wote waliozaliwa kabla ya
saa 6 usiku wa kuamkia siku ya sensa na watu wote waliokufa baada ya saa 6
usiku wa kuamkia siku ya sensa wanastahili kuhesabiwa na wana vipengele ama
sehemu zao za kujaziwa.
Watu gani hawastahili
kuhesabiwa wakati wa sensa?
Sio kila mtu ana haki ya kuhesabiwa
wakati wa zoezi la sensa, kwani wapo ambao zoezi hili haliwahusu kutokana na
kuonekana watachangia kupoteza lengo zima la sensa ambalo ni kupata takwimu
sahihi za idadi ya watu na makazi.
Watu ambao hawastahili kuhesabiwa ni
watoto waliozaliwa baada ya saa 6 usiku wa kuamkia siku ya sensa na wale wote
walikufa kabla ya saa 6 usiku wa kuamkia siku ya sensa.
Pia watu ambao wanaishi nje ya nchi
lakini kazi na shughuli za kikazi kuvuka mipaka na kuingia nchini kufanya kazi
kila siku na kila jioni hurudi nchini kwao hawatastahili kuhesabia.
Halikadhalika kuna Watanzania wote
ambao wako nchi za nje na ambao hawakulala nchini usiku wa kuamkia siku ya
sensa .
Post a Comment