Mpatanishi wa Umoja wa Afrika, Thabo Mbeki,
ametangaza mapatano baina ya Sudan na Sudan Kusini kuhusu malipo ya
mapato ya mafuta baada ya mzozo wa miezi kadhaa, ambao ulikaribia
kuingiza mataifa hayo mawili vitani.
Sudan na jirani yake hawakusema kitu hadi sasa.
Sudan Kusini ilisitisha usafirishaji wa mafuta kupitia Sudan mwezi wa Januari, kufuatia mzozo kuhusu ada iliyokuwa ikitozwa na serikali ya Khartoum.
Post a Comment