Wachezaji na viongozi wa Yanga watasafiri
kwenda Dodoma, kwa ajili ya mwaliko wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, wapenzi wa klabu hiyo, Jumatatu.
Wabunge hao, wamewaalika wachezaji wa Yanga, baada ya kutwaa
taji la Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame,
Jumamosi iliyopita, wakiifunga Azam FC mabao 2-0 kwenye fainali, Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Julai 15, mwaka huu, Yanga ilipata viongozi wapya, ambao ni
Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu wake, Clement Sanga na Wajumbe wanne wa Kamati
ya Utendaji, Abdallah Bin Kleb, George Manyama na Mussa Katabaro.
Hao wanaungana na Wajumbe wengine waliosalia kutoka uongozi
uliochaguliwa mwaka juzi, Mohamed Bhinda, Titto Osoro, Salim Rupia na Sarah Ramadhan,
baada ya wajumbe wengine, wakiwemo Mwenyekiti, Wakili Lloyd Nchunga na Makamu
wake, Davis Mosha kujiuzulu.
Post a Comment