Mshambuliaji
wa kimataifa kutoka timu ya Olympic Atletico ya Burundi, Didier
Kavumbagu amewasili jana usiku na kujiunga na kikosi cha mabingwa wa
Afrika Mashariki na Kati Young Africans Sports Club tayari kwa kuanza
kuitumikia timu yake mpya.
Didier
Kavumbagu aliyechezea timu ya Olympic Atletico katika mashindano ya
Kagame ya mwaka huu na kuifikisha timu yake hatua ya Robo Fainali, kabla
ya kutolewa na timu ya URA ya Uganda.
Pamoja na timu
yake kutolewa katika hatua ya robo fainali, Didier aionyesha kiwango cha
hali ya juu ikiwa ni pamoja kufunga mabao yote mawili katika mchezo wa
kwanza wa Ufunguzi wa mashindano ya Kagame dhidi ya Young Africans.
Mchezaji huyu wa
timu ya Taifa ya Burundi amesajliwa kuichezea timu ya Young Africans
kwa mkataba wa miaka miwili ambapo atakua mitaa ya twiga na jangwani
mapaka mwishoni mwa msimu wa 2013-2014.
Kavambagu
alizaliwa tarehe 02/05/1988 mjini Bujumbura na kuanza kucheza soka
katika timu za mitaani kabla ya kuchaguliwa timu ya taifa ya vijana U-17
mwaka 2006 na kushiriki mashindano ya kombe la vijana CECAFA U-17
visiwani Zanzibar.
Alionyesha
kiwango cha hali ya juu katika mashindano hayo na kupelekea kusajiliwa
na timu ya Olympic Atletico ambapo ameitumikia mpaka mwaka huu alipoamua
kuachana na yo na kujiunga na mabingwa wapya wa kombe la Kagame Young
Africans Sports Club.
Young Africans
imeanza jana mazoezi yake kwa ajiliya kujiandaa na msimu mpya wa ligi
kuu Tanzania bara unaotazamiwa kuanza septemba mosi, na wachezaji wote
wamehudhuria mazoezi jana na leo Didier amejumuika na wachezaji wenzake
kufanya mazoezi chini ya kocha Mkuu Tom Saintfiet katika uwanja wa shule
ya sekondari Loyola.
Post a Comment