![]() |
Kelvin Yondan |
Na Princess Asia
KAMATI
ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana
Jumapili (Septemba 2 mwaka huu) kupitia usajili wa wachezaji kwa msimu
wa 2012/2013.
Usajili
utakaopitiwa ni wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Lidi Daraja la
Kwanza (FDL) ambapo Kamati itapitia pingamizi zilizowasilishwa na klabu
mbalimbali dhidi ya wachezaji waliosajiliwa na klabu zingine.
Miongoni
mwa masuala yanayotarajiwa kujadilika katika kikao hicho ni usajili wa
beki Kevin Yondan kutoka Simba kwenda Yanga na usajili wa kiungo
Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kutoka Azam FC kwenda Simba SC.
Ni
kesi zinazofanana- kwa Redondo anadaiwa kusaini Simba wakati bado
hajamaliza mkataba wake Azam FC sawa na Yondan, anadaiwa kusaini Yanga
wakati bado ana mkataba na klabu yake, Simba SC.
Wachezaji
wote wawili wamekanusha kuwa na mikataba na klabu zao za awali na
Kamati ya Mgongolwa inatarajiwa kutoa jibu juu ya mustakabali wa
wachezaji hao msimu ujao watacheza wapi.
chanzo: Binzubeir Blog
Post a Comment